Simba barua yenu ya kugomea mechi ina mkanganyiko mkubwa,,mjitafakari kabla hayajawakuta

Simba barua yenu ya kugomea mechi ina mkanganyiko mkubwa,,mjitafakari kabla hayajawakuta

Tabu ipo wapi?

Simba imeona kuna mazingira yanayohatarisha mchezo kuwa fair kwa upande wa Simba, kama imekosea kanuni Yanga itapewa hizo P3 wanazozitaka sana mpaka wanazuia mazoezi.

NO REFORM NO DERBY.

Utaratibu uwe huu huu mpaka derby iwe huru.
Duh!! Dabi iwe huru kivipi? Mnatafuta kichaka cha kujifichia?
 
Mabaunsa ndio wasimamizi wa uwanja? Ndio Wenye funguo za uwanja wa taifa? Wangeingiaje kama mageti yamefungwa?
hahaha ndugu kwahyo hata ukikuta mabaunsa wameshika silaha za moto pale getini wameweka kizuizi ni sawa tu sababu sio washika funguo na si makamisaa wa mchezo!! Kinacholalamikiwa hapa ni vurugu zilizofanywa na wenyej wakiwatuhumu kwa nadharia za uchaw kwa kitu ambacho hakina uthibitisho na ikapelekea kushindwa kufanya mazoez ya mwisho siku moja kabla ya mchezo kwa mgeni wa mchezo kikanuni kwa kutokuwepo kwa usalama eneo la uwanja. Au napo si sawa?
 
We
Kwaiyo Simba anaruhusiwa kugomea mechi? Nimekwambia tuwekee kanuni inayosema akizuiwa kufanya mazoezi agomee mechi
Yanga mbona uligomea muda wa saa Moja kusogezwa mbele
 
Kwamba mabaunsa hao mnaowaita wa yanga ndio waliokua na ufunguo wa kuingia ndani ya uwanja? Niliona gari ya polisi imebock njia kabisa ili gari ya simba isisogee getini.

Kwa kifupi inaonekana hapakua na mawasiliano kati ya simba na meneja wa uwanja
Gentleman!
Litajulikana wakati wa maamuzi.

Usiwe na haraka.
 
We

Yanga mbona uligomea muda wa saa Moja kusogezwa mbele
Walikuwa sahihi kwakuwa taarifa ilitoka nje ya muda kikanuni,,uwezi kuahirisha mechi ghafla ghafla tu kama ndondo cup lazima Kuna muda unatakiwa utoe taarifa ya kusogeza muda
 
Yanga si

uligomea mechi kusogezwa mbele saa moja
Yanga haikogomea mechi Sheikh! Badala yake ilifika uwanjani muda uliopangwa wa saa 10 na kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili kabla ya mechi, badala ya ule muda wa mchongo wa saa 1 jioni.
 
Ila Simba unaona haipo sahihi kugomea mechi kwa sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi
Walikuwa sahihi kwakuwa taarifa ilitoka nje ya muda kikanuni,,uwezi kuahirisha mechi ghafla ghafla tu kama ndondo cup lazima Kuna muda unatakiwa utoe taarifa ya kusogeza muda
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Barua hii iliyoandikwa na Simba Ina mkanganyiko sana sijui wamekurupuka ama vipi,,nimeisoma vizuri mstari baada ya mstari na nimeona wamejichanganya pakubwa!
Kwanza nukuu ya kwanza hii hapa;-

1) Nukuu''katika sintofahamu iyo Simba iriarifiwa na meneja wa uwanja kuwa hana maelekezo ya kamishna wa mchezo'' kupitia mstari huu ni wazi kuwa Simba awajazuiliwa kuingia uwanjani na mabaunsa kama walivyoainisha kwenye barua yao bali wamezuiliwa na meneja wa uwanja kwani ndie mwenye mamlaka na funguo za mageti ya uwanja kuruhusu watu waingie uwanjani!

2) Nukuu ya pili " Mabaunsa wa klabu ya yanga walivamia msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu na wakizuia msafara wa Simba kuingia uwanjani kufanya mazoezi" kupitia mstari huu pia Simba wameandika juu ya mabaunsa wa yanga sasa hapa najiuliza wamejuaje kwamba wale ni mabaunsa wa yanga? Ni uthibitisho upi walioutumia kung'amua kwamba wale ni mabaunsa wa yanga? Pale akukuwepo na kiongozi yeyote wa YANGA,,

Je, walikuwa na vitambulisho? Ama jezi za yanga? Viongozi wote wa yanga wamesajiliwa TFF kikanuni na Sheria za Mpira zinavyotaka akuna sehemu yanga wamesajili jina la baunsa!

Lakini pia barua ya Simba inasema mabaunsa wa yanga wamezuia timu kuingia uwanjani wakati ukiangalia Ile video lile tukio watu walikuwa nje ya uwanja Ina maana na wao awakuwa na mamlaka ya kuingia ndani ya uwanja kwakuwa meneja wa uwanja alipiga rock!

Mabaunsa wanawezaje kumzuia mtu asiingie uwanjani wakati uwanja wenyewe umefungwa?
Simba nawashauri mpeleke timu uwanjani na adhabu za kikanuni uamuliwa kikanuni na sio kugomea mechi vinginevyo point 3 na magoli 3 itakuwa ni halali ya yanga!

Kama mganga wenu aliwapa masharti magumu na mkaona imebuma vilio vingekuwa vingi muwaambie ukweli wanachama wenu na sio kichaka cha ukizuiwa kufanya mazoezi,,mbona yanga mechi iliyopita ilizuiwa kufanya pale mazoezi kwanini awakugomea mechi?
Hawa ndio wanasheria wa Utopolo ambao Kila uchwao wanashindwa kesi
 
Ila Simba unaona haipo sahihi kugomea mechi kwa sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi
Yanga wiligoma na kanuni ilikuwa upande wao,,Simba ni kanuni ipi Iko upande wao?
 
Hawa ndio wanasheria wa Utopolo ambao Kila uchwao wanashindwa kesi
Wewe na wenzako mbumbumbu msipotuwekea kanuni hapa inayowataka mgomee mechi eti kwa kuzuiwa kufanya mazoezi tutaendelea kudhibitisha maneno ya Rage!
 
Ingekuwa huru kusingekuwa na kuzuiana kufanya mazoezi.
Kabisa unashabikia simba kugomea game kisa hajaingia usiku uwanja ambao ni nyumbani kwake? Acheni zengwe nyie watu. Yanga sio mmiliki wa ule uwanja hata kama kikanuni yeye ni mwenyeji wa mchezo. Pale walipokua wanazuiwa simba, hapakua na kiongozi wa Yanga hata mmoja. Meneja wa uwanja hakuwa na taarifa. Kama mlipeleka timu bila kuwataarifu wenye kuusimamia uwanja mlitaka mbembelezwe.? Acheni utoto huo
 
Jiridhishe na kanuni basi boss zinazohusiana na tafsiri ya uwenyeji na ugeni wa mechi kabla hujajibu.

Pia fuatilia majibu ya viongozi wa ligi kuhusu hii hoja yako. Mwenyekiti wa bodi ya ligi aliulizwa hili swali unalolijibu hapa bila kujua tafsiri za kanuni zilizopo na kalijibu vizuri tu. Kuna mdau kaweka hayo mahojiano hapa JF.
 
Kwahiyo wanaamua kususa kisa hawajaruhusiwa na meneja wa uwanja kuingia kufanya mazoezi? Ule uwanja una utaratibu wake na sio uwanja wa club ya yanga. Kususia game, ni umama na kutaka kudeka. Mbona Yanga hawakususia game iliyopita
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Derby haina kipengele labda kipengele waje nacho makolo
 
Back
Top Bottom