Simba barua yenu ya kugomea mechi ina mkanganyiko mkubwa,,mjitafakari kabla hayajawakuta

Duh!! Dabi iwe huru kivipi? Mnatafuta kichaka cha kujifichia?
 
Mabaunsa ndio wasimamizi wa uwanja? Ndio Wenye funguo za uwanja wa taifa? Wangeingiaje kama mageti yamefungwa?
hahaha ndugu kwahyo hata ukikuta mabaunsa wameshika silaha za moto pale getini wameweka kizuizi ni sawa tu sababu sio washika funguo na si makamisaa wa mchezo!! Kinacholalamikiwa hapa ni vurugu zilizofanywa na wenyej wakiwatuhumu kwa nadharia za uchaw kwa kitu ambacho hakina uthibitisho na ikapelekea kushindwa kufanya mazoez ya mwisho siku moja kabla ya mchezo kwa mgeni wa mchezo kikanuni kwa kutokuwepo kwa usalama eneo la uwanja. Au napo si sawa?
 
We
Kwaiyo Simba anaruhusiwa kugomea mechi? Nimekwambia tuwekee kanuni inayosema akizuiwa kufanya mazoezi agomee mechi
Yanga mbona uligomea muda wa saa Moja kusogezwa mbele
 
Kwamba mabaunsa hao mnaowaita wa yanga ndio waliokua na ufunguo wa kuingia ndani ya uwanja? Niliona gari ya polisi imebock njia kabisa ili gari ya simba isisogee getini.

Kwa kifupi inaonekana hapakua na mawasiliano kati ya simba na meneja wa uwanja
Gentleman!
Litajulikana wakati wa maamuzi.

Usiwe na haraka.
 
Yanga si
Simba ina wakati mgumu. Walifikiri wataenda kuroga, meneja akaamua kuwabania. Sasa wakubali tu leo ni ubaya ubwela. Na hakuna kususia mechi kwa sababu za kipuuzi.
uligomea mechi kusogezwa mbele saa moja
 
We

Yanga mbona uligomea muda wa saa Moja kusogezwa mbele
Walikuwa sahihi kwakuwa taarifa ilitoka nje ya muda kikanuni,,uwezi kuahirisha mechi ghafla ghafla tu kama ndondo cup lazima Kuna muda unatakiwa utoe taarifa ya kusogeza muda
 
Yanga si

uligomea mechi kusogezwa mbele saa moja
Yanga haikogomea mechi Sheikh! Badala yake ilifika uwanjani muda uliopangwa wa saa 10 na kufanya mazoezi ya utimamu wa mwili kabla ya mechi, badala ya ule muda wa mchongo wa saa 1 jioni.
 
Ila Simba unaona haipo sahihi kugomea mechi kwa sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi
Walikuwa sahihi kwakuwa taarifa ilitoka nje ya muda kikanuni,,uwezi kuahirisha mechi ghafla ghafla tu kama ndondo cup lazima Kuna muda unatakiwa utoe taarifa ya kusogeza muda
 
Reactions: BRN
Hawa ndio wanasheria wa Utopolo ambao Kila uchwao wanashindwa kesi
 
Ila Simba unaona haipo sahihi kugomea mechi kwa sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi
Yanga wiligoma na kanuni ilikuwa upande wao,,Simba ni kanuni ipi Iko upande wao?
 
Hawa ndio wanasheria wa Utopolo ambao Kila uchwao wanashindwa kesi
Wewe na wenzako mbumbumbu msipotuwekea kanuni hapa inayowataka mgomee mechi eti kwa kuzuiwa kufanya mazoezi tutaendelea kudhibitisha maneno ya Rage!
 
Ingekuwa huru kusingekuwa na kuzuiana kufanya mazoezi.
Kabisa unashabikia simba kugomea game kisa hajaingia usiku uwanja ambao ni nyumbani kwake? Acheni zengwe nyie watu. Yanga sio mmiliki wa ule uwanja hata kama kikanuni yeye ni mwenyeji wa mchezo. Pale walipokua wanazuiwa simba, hapakua na kiongozi wa Yanga hata mmoja. Meneja wa uwanja hakuwa na taarifa. Kama mlipeleka timu bila kuwataarifu wenye kuusimamia uwanja mlitaka mbembelezwe.? Acheni utoto huo
 
Jiridhishe na kanuni basi boss zinazohusiana na tafsiri ya uwenyeji na ugeni wa mechi kabla hujajibu.

Pia fuatilia majibu ya viongozi wa ligi kuhusu hii hoja yako. Mwenyekiti wa bodi ya ligi aliulizwa hili swali unalolijibu hapa bila kujua tafsiri za kanuni zilizopo na kalijibu vizuri tu. Kuna mdau kaweka hayo mahojiano hapa JF.
 
Kwahiyo wanaamua kususa kisa hawajaruhusiwa na meneja wa uwanja kuingia kufanya mazoezi? Ule uwanja una utaratibu wake na sio uwanja wa club ya yanga. Kususia game, ni umama na kutaka kudeka. Mbona Yanga hawakususia game iliyopita
 
Reactions: Tsh
Derby haina kipengele labda kipengele waje nacho makolo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…