Simba bingwa Kagame Cup.....!!!

Simba bingwa Kagame Cup.....!!!

Aaaah hasirraaaa jamaaa wametufunga 2-1 siamini kabisa...Huyu Rage kaja na mikosi nini wapi Dalali?
 
Ila tumetinga robo fainali kwa tofauti ya magoli....Sasa huenda tukakutana na TP Mazembe ama APR nasiki harufu ya kipigo kama ndio hivi.
 
Isije ikawa kuna kamgomo baridi! Simba sio timu ya kupoteza mechi mfululizo kwenye michuano kama hii. Hebu viongozi walioko Kigali wakae na wachezaji wajue kuna nini hasa wajaribu kutatua kabla ya hizo mechi za quarter final.
 
:target::target::target::target:....................mwaka wa hasara umeanza!!
 
Isije ikawa kuna kamgomo baridi! Simba sio timu ya kupoteza mechi mfululizo kwenye michuano kama hii. Hebu viongozi walioko Kigali wakae na wachezaji wajue kuna nini hasa wajaribu kutatua kabla ya hizo mechi za quarter final.

Mgomo baridi wapi,sisi tunawasubiri nyumbani
 
Isije ikawa kuna kamgomo baridi! Simba sio timu ya kupoteza mechi mfululizo kwenye michuano kama hii. Hebu viongozi walioko Kigali wakae na wachezaji wajue kuna nini hasa wajaribu kutatua kabla ya hizo mechi za quarter final.
Hili ndio tatizo lenu kubwa. Kuji-overate!!!
Hata hivyo mnayo nafasi kama mtakuwa wapole na kwenda kuwapigia magoti watani pale Jangwani wawape mbinu waliwezaje kuchukua ubingwa pale Kampala miaka kadhaa iliyopita pamoja na kuanza michuano kwa kusuasua hivihivi kama mlivyoanza ninyi!!
 
Wadau na wapenzi wa michezo...leo wawakilishi pekee waingia uwanjani kutuwakilisha na APR....tuungane katika dua na sala ili ushindi upatikane!! Mungu ibariki SIMBA, Mungu ibariki TANZANIA.....................
 
duh kwa mwenendo wa simba safari hii naogopa hata kujua matokeo jamani any way Mungu saidia mnyama ishinde
 
Jamani mechi ya leo na wanajeshi vipi? Hata kama tumefungwa anikeni matokeo hapa.. pls
 
Mpaka dk ya 75 matokeo yalikuwa 1 - 1, kwa mujibu wa mtu wangu anayeishuhudia mechi kule Kigali. Akinipa matokeo ya mwisho nitayabandika humu mara moja!
 
Back
Top Bottom