Simba Day: Simba S.C 4 AFC Leopards 0

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
SIMBA SC imesherehekea vyema miaka 80 jioni ya leo baada ya kuifunga AFC Leopard ya Kenya mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Ibrahim Hajib Migomba ameendelea kumvutia kocha mpya, Mcameroon Joseph Marius Omog baada ya kufunga mabao mawili, huku wachezaji wapya, Mrundi Laudit Mavugo na Shizza Kichuya wakifunga pia.

Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Hajib dakika ya 38 kwa shuti la umbali wa mita takriban 30 baada ya kupokea pasi ya kiungo Mkongo, Mussa Ndusha.

Mabadliko ya karibu nusu kikosi yaliyofanywa na kocha Omog, anayesaidiwa na Mganda, Jackson Mayanja kipindi cha pili yaliisaidia Simba kupata mabao matatu.
Hajib alimalizia vizuri krosi ya Kichuya kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 56 na dakika 58 Jamal Mnyate akapoteza nafasi nzuri aliyotengenezewa na Mavungo.

Lakini Kichuya akawainua vitini mashabiki wa Simba SC walioongozwa na Rais wa klabu, Evans Elieza Aveva na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kufunga bao la tatu dakika ya 66, akimalizia krosi ya Mavugo.

Mavugo aliyejiunga na Simba SC mwishoni mwa wiki, akaifungia Simba SC bao la nne dakika ya 82
akiunganisha krosi nzuri ya Kichuya, aliyekuwa nyota wa mchezo wa leo.
Mchezo wa leo uliokwenda sambamba na sherehe za miaka 80 ya klabu, maarufu kama Simba Day, ulihudhuriwa pia na mfanyabishara Mohammed Dewji ambaye ametoa ofa ya kuinunua klabu hiyo kwa Sh. Bilioni 20.

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Janvier Besala Bokungu/Hamad Juma dk72, Novaty Lufunga, Method Mwanjali/Juuko Murshid dk77, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Jamal Mnyate dk46, Mussa Ndusha/Muzamil Yassin dk46, Frederick Blagnon/Laudit Mavugo dk46, Ibrahim Hajib/Mohamed Ibrahim dk67 na Shizza Kichuya.

AFC Leopards; Ian Otieno, Cresten Mwanzo, Bernard Mangoli, Edwin Wafula, Eugine Ambulwa, Joshua Mawira, Bernard Ongoma, Yusuf Suf Sozi, John Ndirangu, Paul Kiongera/Andrew Toloiwa dk66 na Jack Kiyai/Simon Abuko.

Source: "adui wa Ndala" Bin Zubeiry.
 
Hivi simba alishawahi kufungwa kwenye simba day???
 
ile timu ya hal
mashauri iliyokupiga juzi kwa nini hujaialika simba day ukaialika mchangani ya Kenya?
 
Tuseme kweli hao Leopards ni wakudharau kweli? Endeleeni kujifariji,simba hii siyo ya mwaka jana.
 
Ghana na Kenya ni kama mbingu na ardhi "mbojo" hivi ni lini Leopard imekuwa bingwa Kenya au inashikilia kombe gani au mngeomba mechi na timu kama Azam, Prison,Mwadui kuliko hiyo Leopard!!! Ngoja tuone maajabu kwani KMC walifanya nini Morogoro? Timu daraja la kwanza
 
Hivi simba alishawahi kufungwa kwenye simba day???
YEAH,ILISHAWAHI KUFUNGWA NA MBABE WAKE URA YA UGANDA MWAKA 2012,IKAFUNGWA TENA NA URA MWAKA ULIOFUATA 2013 KABLA YA KUIICHAPA 2014
 
YEAH,ILISHAWAHI KUFUNGWA NA MBABE WAKE URA YA UGANDA MWAKA 2012,IKAFUNGWA TENA NA URA MWAKA ULIOFUATA 2013 KABLA YA KUIICHAPA 2014
Asante kwa kumbukumbu mkuu, hivi afc Leopard kwenye ligi yao wapo nafasi ya ngap vilee??
 
Naona watu mnajadili matokeo zaidi kuliko lengo kuu la siku hii ya Simba Day. Ni siku ya kutambulisha kikosi, jezi zao na kusherehekea kumbukumbu ya miaka 80. Hiyo mechi ilikuwa ni kwa ajili ya burudani tu, msitoe mimacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…