Simba funueni timu yenu ya vijana itawasaidia

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ninapoona Simba wanahangaika kusajili wachezaji wa kigeni ambao ni dhahiri wanakuja kuwa wachezaji wa akiba maana namba zao tayari zina wachezaji tegemeo, naona ni matumizi mabaya ya rasilimali. Hawa wachezaji wa akiba kwa kiasi kikubwa wangekuwa ni wazawa na wale wenye uwezo wapewe nafasi timu kubwa.

Simba wangejitahidi kutafuta vijana kama 15 hivi, makocha Juma Mgunda na Selemani Matola wakapelekwa kuwasimamia na kuwaendeleza, kila mwaka timu isingeweza kukosa wachezaji 4 wenye uwezo wa kuwapandisha ngazi. Wengine wangekuwa wanauzwa ndani na nje ya nchi.

Pia changamoto za mchezaji mmoja mmoja kama ilivyo sasa kwa Denis Kibu na Habib Kyombo zingeweza kutatulika kwa kuwapeleka wachezaji wa namna hii wafanye mazoezi kwa uangalizi maalumu katika timu ya vijana kwa muda fulani. Hii itasaidia kuangalia madhaifu ya mchezaji na kuyarekebisha kabla hajarudishwa kikosini.

Ni vigumu kocha mkuu kurekebisha madhaifu ya mchezaji mmoja mmoja, hasa yale ya msingi yasiyohusiana na mfumo anaojenga wakati huo huo anahangaika kujenga mfumo ndani ya timu nzima.
 
Hiyo timu itachelewa sana kuchukua ubingwa wowote ule wa maana iwapo itaendelea kuwakumbatia wachezaji wazee.
 
Mods ingependeza mngerekebisha title ya uzi huu isomeke "fufueni" badala ya "funueni"

Mhariri Active
 
Kwenye hili tunapuyanga. Mara ya mwisho kuona under 20 anapanda na ku shine ni enzi za kina Mkude, Ndemla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…