Simba haikufanya mazoezi uwanja wa Jamhuri Morogoro ikapoteza mechi muhimu

Simba haikufanya mazoezi uwanja wa Jamhuri Morogoro ikapoteza mechi muhimu

Kuna watu wanachukulia poa utaratibu na haki iliyopewa timu ngeni kufanya mazoezi katika uwanja utakaochezewa mechi siku moja kabla ya mechi.

Wachezaji wanapokuwa wamefanya mazoezi katika uwanja wa vita watakaoenda kuutumia, hili ni suala la kiufundi na linasaidia kuandaa wachezaji kimwili na kisaikolojia. Lengo kuu ni kuweka mizania sawa kati ya timu zote mbili kuelekea mchezo husika. Kumbuka football inaendeshwa na dhana nzima ya "fair play" na kanuni nyingi zimetengenezwa kulinda dhana hii.

Nakumbuka misimu miwili iliyopita Simba ilifanya kosa moja kubwa sana lililoigharimu timu na kufifisha harakati zake za ubingwa.

Simba ilihamishia mechi yake dhidi ya Prisons katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro na kupoteza mchezo ule kwa goli 1-2. Sikumbuki sababu hasa ilikuwa nini ila pamoja na kwamba ilikuwa ndiyo mwenyeji wa mchezo, Simba haikufanya mazoezi katika uwanja ule wa Jamhuri kabla ya mchezo husika. Nakumbuka kulaumu kuwa moja ya sababu ya Simba kupoteza mchezo ule hii inaweza kuwa ilichangia pakubwa sana.

Utagundua issue siyo kuwa mwenyeji bali kuwa na familiarity na uwanja husika na kuutumia muda mfupi kabla ya mechi ni jambo muhimu kwa wachezaji wa timu zote mbili.

Kwa kulipanua zaidi hili suala na kuongeza uelewa, ndiyo maana mara nyingi utaona Simba huwa inaendana mwanzaa kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa walau siku moja kabla ya mechi za kimataifa na pia huwa inafanya hivyo pia katika uwanja wa KMC kabla ya mechi ya ligi. Hili ni suala la kiufundi zaidi na usipokuwa mtu wa mpira hauwezi kulielewa.

NYONGEZA: Hapa sijaongelea ukweli kuwa kuizuia timu iliyo na haki ya kutumia uwanja siku moja kabla ya mechi ni kuvuruga ratiba yake ya maandalizi ya mechi husika na inaua dhana nzima ya fair play. Ukiizuia timu kama ilivyotokea kwa Simba, itatakiwa kwenda katika mechi bila kuwa imefanya mazoezi kwa masaa 48. Hapo utimamu wa kimwili wa wachezaji utakuwaje?
Na mwanza
 
Tatizo mnadekezwa saa kumbe mpaka huku kwenye soka la wanawake mnadeka. Tabia za kudeka mmezitoa kwenye soka la wanawake mmezileta kwenye soka la wanaume.
Mechi ilisogezwa mbele masaa mawili tu Yanga ikagoma kucheza ila cha ajabu timu inazuiwa kufanya mazoezi muhimu mnataka ionekane ni jambo la kawaida.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Toka lini ukaona Yanga ana walinzi?
Kwanini Simba hawakupoga simu hapo Chang'ombe police station waje kuwaondoa hao waharifu na wafanye mazoezi
Mkuu, Haya majibu mbona yote yapo kwenye taarifa ya bodi ya ligi kuhairisha mechi, umeisoma?
 
Mechi ya Simba na Azam imechezwa siku 12 zilizopita. Wataalamu wangekuwa na akili kisoda kama zako wangesema haki itolewe kwa kwanza kuangalia ni lini mara ya mwisho timu ilitumia uwanja husika. Badala yake kanuni ipo wazi na clear na kanuni lazima ziheshimiwe maana hazijatungwa kujaza tu makaratasi.
Kwa Nini mnaishia kwenye haki tu ya kufanya mazoezi hamtaki kuelezea wajibu wa kutoa taarifa Kwa mwenyeji, meneja na Afisa wa Mechi!!! Kila haki Ina wajibu je wajibu wenu mliutimiza wa kutoa Taarifa!!?
 
Mechi ilisogezwa mbele masaa mawili tu Yanga ikagoma kucheza ila cha ajabu timu inazuiwa kufanya mazoezi muhimu mnataka ionekane ni jambo la kawaida.
Yanga alifika kwenye mechi muda wa awali uliopangwa na Simba hakutokea
 
Mkuu, Haya majibu mbona yote yapo kwenye taarifa ya bodi ya ligi kuhairisha mechi, umeisoma?
Taarifa ya bodi ya ligi inasema Simba hakuwapa taarifa za ujio wao Kwa meneja wa uwanja, kamshina wa michezo wala mwenyeji wa mchezo
Sasa ulitaka Simba apokelewe na nani hapo kiwanjani?
 
Mechi ilisogezwa mbele masaa mawili tu Yanga ikagoma kucheza ila cha ajabu timu inazuiwa kufanya mazoezi muhimu mnataka ionekane ni jambo la kawaida.
Mechi gani hii,kwa hii ya ya JKT umeamua kuichunia,imetokea mwaka jana 2024.

Kwani kuna kanuni inayo ruhusu timu kususa baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi baada ya mechi?Nitajie kifungu.....

Kikanuni Yanga alikuwa sawa kipindi kile bodi ya ligi ilibadilisha mda wa mechi siku ya mechi husika, Yanga hawakupata taarifa OFFICIALLY wakaenda uwanjani baada ya dk 15,hamkutokea wakaondoka uwanjani. Kama kawaida ukatumika uchochoro wa HEKIMA NA BUSARA zikaachwa kanuni.
 
Taarifa ya bodi ya ligi inasema Simba hakuwapa taarifa za ujio wao Kwa meneja wa uwanja, kamshina wa michezo wala mwenyeji wa mchezo
Sasa ulitaka Simba apokelewe na nani hapo kiwanjani?
Ilipokelewa na watu wanaodhaniwa ni nani na kuzuiwa? Usijibu unachofikiri, soma taarifa ya bodi.
 
Kwa Nini mnaishia kwenye haki tu ya kufanya mazoezi hamtaki kuelezea wajibu wa kutoa taarifa Kwa mwenyeji, meneja na Afisa wa Mechi!!! Kila haki Ina wajibu je wajibu wenu mliutimiza wa kutoa Taarifa!!?
Kanuni inasema Afisa wa mechi ndiyo anatakiwa atoe taarifa pale kunapokuwa na mazingira ya kanuni hiyo itashindwa kufanya kazi! Badala yake mabausa wa Yanga wakajipa jukumu lisilo lao na sasa msala mnao.

Hiyo haki ya timu ngeni ni automatic haina mjadala na pale inakuwa haiwezekani kutekelezeka ndiyo inabidi timu husika itaarifiwe mapema. Swali lako linatakiwa kuwa je Simba ilitaarifiwa mapema kuwa haitaweza kutumia uwanja wa Mkapa kufanya mazoezi?
 
Mkishavurunda mnatafuta sketi za kujifichia. Juzi mlikana "makolo" siyo Simba, leo hii mnawakana watendaji wenu mnaowatuma kufanya uhuni.
Bro usilete stori za kwenye vijiwe cha kahawa, watanzania wa yanga wanajulikana mtendaji gani alieizuia simba kuingia uwanjani ? Let's maneno
 
Hao watu Gani wataje?
Screenshot_20250309-110318_Chrome.jpg
 
Bro usilete stori za kwenye vijiwe cha kahawa, watanzania wa yanga wanajulikana mtendaji gani alieizuia simba kuingia uwanjani ? Let's maneno
Kwa nini nishangae mnavyowaruka watendaji wenu wakati juzi mmeishangaza dunia kwa kudai "Makolo" ni timu ya mtaani na haihusiani na timu yoyote ya NBC. Baada ya hapo ni nani atawachukulia siriazi?
 
Kwa Nini mnaishia kwenye haki tu ya kufanya mazoezi hamtaki kuelezea wajibu wa kutoa taarifa Kwa mwenyeji, meneja na Afisa wa Mechi!!! Kila haki Ina wajibu je wajibu wenu mliutimiza wa kutoa Taarifa!!?
Wanaojua sheria za mpira wanielimishe, Je ni kweli kwamba sheria huwa inasema timu mwenyeji huwa ana kabidhiwa uwanja siku moja kabla ya mechi kuchezwa ?
 
Back
Top Bottom