Simba haikugomea mechi

pakaywatek

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
4,660
Reaction score
6,282
Nimekua nikisoma kwenye mitandao kuwa Simba iligomea mechi mimi nakataa na sababu zangu ni kwamba mechi haikuchezwa.

Hili mgomo uhalalishwe ni pale bodi ya ligi ingeendelea na msimamo wake wa awali kuwa mechi ipo palepale afu wapeleke waamuzi na kamisaa uwanjani na waisubiri simba dakika 30 na simba wasitie timu afu wamalize mchezo hapo ndipo pangekua na mjadala wa mgomo.

Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Sasa Simba kwa hasira zao wakapost usiku kuwa wamesusia mechi asubuhi badi ya ligi wanasema mechi ipo palepale kabla ya saa za mchezo bodi ya ligi inatangaza tena hakuna mechi, sasa simba wangeenda uwanjani si wangekua kituko kama wale wengine!!.

We umeambiwa hakuna mechi na aliyekuambia ni mwenye mehi mwenyewe afu unapeleka timu uwanjani "UTOTO" wahed.

Simba hawakugoma bali mechi ilihairishwa mpaka SIMBA NA YANGA wajenge viwanja vyao.
 
Unalazimisha iwepo tofauti ya kususia na kugoma
 
ni kweli; haikugomea mechi bali iliingia mitini. Iliona ni heri lawama kuliko kutembezewa kichapo. Safari hii kilikuwa kinafikia sita
 
Kasome barua ya Simba waliyopost kabla ya tamko lolote la bodi ya ligi,,walikuwa na mamlaka Gani ya kutoa official statement kwamba awapeleki timu uwanjani kabla ya kuwasiliana na bodi ya ligi na bodi ya ligi ndio ingetoa statement yenyewe kwanza juu ya mechi husika na sio Simba!
 
Mechi iliahirishwa na Bodi ya Ligi, itapangiwa tarehe nyingine, maelezo yoyote tofauti na haya ni uropokaji na kupotezeana muda tu, ambaye hata leta timu uwanjani siku ya mechi ndiye atakuwa amegomea na sheria itafuata mkondo wake.
 
Wakati fulani nimegundua bora lawama tu kuliko fedheha. Yaani unaona kabisa mbele yako kuna maafa, halafu ujipeleke mzima mzima ukaangamie! Hapo ni kutimua mbio tu ili ukajipange upya.
 
Achana na mpira wa kipuuzi wa Tanzania, ni upumbavu kuwa serious na mpira wa Tanzania, huo muda uluotumia kusoma haya mambo ya mpira wa Tz, Bora ungeutumia kujifunza mambo ya AI au Crypto.
 
Yanga Wamesema 'WATAGOMEA' mechi ....!

Na Wataenda CAS.....! Patrick Mwanasheria Wa Yanga ndo atasimamia shoo.
Ila najua bodi ya Ligi watampeleka Wakili msomi Bernard Morison
 
Mechi iliahirishwa na Bodi ya Ligi, itapangiwa tarehe nyingine, maelezo yoyote tofauti na haya ni uropokaji na kupotezeana muda tu, ambaye hata leta timu uwanjani siku ya mechi ndiye atakuwa amegomea na sheria itafuata mkondo wake.
Hakunaga mpira wa hivyo kwamba timu itacheza itakapo jisikia
 

Kweli hawaja gomea.
 
Ngoja tusubiri tuone kitakachojiri.
Tukiweka mihemuko pembeni kuna kosa limefanyika pande zote tatu ila aliye puyanga zaidi ni bodi ya ligi mara baada ya vurugu kutoea wangetoa tamko kabla ya vilabu kusema lolote sasa wao wanakuja na tamko tayari vilabu visha toa misimamo kuna nini hapo?
 
Hapo ni kujinusa vidole ambavyo una uhakika umevichafua...

Simba waliandika officially kwa bodi ya ligi kuwa hawatapeleka timu uwanjani!

Hata bodi ya ligi isingetoa tangazo lile lililokuwa influenced na Simba, Timu isingeenda uwanjani!

Sasa mmepata kichaka kiufupi cha kuficha sura zenu ( kuwa mechi iliahirishwa na bodi) wakati makalio yenu yananuka huku nje!
 
Pata muda umsikilize huyu jamaa ana akili...

 
Bodi wamelikoroga big time hata sijui watajinasua vipi hapa.
 
Kuandika siyo shida bodi wangesimamia mechi ichezwe ili waone kama simba wamesusa kweli. Sasa mechi imeahirishwa simba waende uwanjani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…