Tukiacha mahaba binafsi ya timu zetu! Tukubali tu Simba bado haina uwezo wa kuifunga Yanga iliyosheheni mastaa kibao kama Aziz Kii, Max Nzengeli, Prince Dube, Clement Mzize, Khalid Aucho, Ibra Baka, Dickson Job, na mastaa wengine wengi!!
Na ndiyo maana hata itokee Yanga ikafungwa, mashabiki wengi hatutegemei kuulaumu uongozi wa timu! Maana umetimiza wajibu wake kwa kusajili wachezaji wazuri. Badala yake lawama zitaenda kwa kocha aidha kwa kupanga kikosi dhaifu, au baadhi ya wachezaji kucheza chini ya kiwango.