Simba hapo vipi??

Simba hapo vipi??

Mleta mada, hapo vipi? Kuna ya kibegi sijui niliipotezea wapi, wengi hawakuishtukia na mimi nikaikaushia

Screen Shot 2023-12-16 at 1.04.15 AM.png
 
Simba hawajielewi, mkutano mkuu unakuwa Kama mko kanisani au msikitini, sijaona mtu yoyote akihoji Ila baada ya siku mbili utasikia watu kwenye redio, magazeti wanaanza kuhoji Mambo ambayo kimsingi yalitakiwa yahojiwe kwenye mkutano mkuu.
Mwaka Jana Simba walitangaza bajeti ya bilioni 13 lakini bada ya yanga kufanya mkutano wao na bajeti kuwa kubwa kuliko ya Simba CEO wake akaibuka na bajeti tofauti kuonyesha Simba Wana bajeti kubwa kuliko yanga kitu ambacho sio cha ukweli.
Simba ilianzisha mchango kwa ajili ya kujenga uwanja, Leo wanasema pesa zimejenga uzio na watu wanapiga makofi lakini wameshindwa kuhoji naninaliyebadilisha matumizi ya hizo pesa na pia Simba Wana mpango gani wa kujenga viwanja.
Mapato ya jengo la Msimbazi Kila mwaka ni milioni 500 hakuna mkakati wowote wa kuyaongeza Wala kujenga jengo la kisasa.
Simba inajisifu kukusanya bilioni 15 lakini umeshindwa kupata udhamini wa benki hata moja pamoja na kuwa na kiasi kikubwa cha pesa.
Mapato ya wadhamini hayajatolewa ufafanuzi hata mkataba wa kuweka logo kifuani kwa mashindano ya Afrika haujawekwa wazi.
Mauzo ya wachezaji mfano Sackho hayajawekwa wazi.
Kikao Kama like kisingechukua muda mfupi yaani hata mafanikio wanayotangaziwa hayaendani na ukubwa wa Simba .
-Matumizi ya hela za kuingia robo na group stage kila mwaka hayapo.
-Hela ya mgawo wa African football league hayapo wazi
-Matangazo ya biashara Mo kifuani hamna maelezo ya maana
-Matangazo ya bahati nasibu mfalme bingwa na shabiki bingwa haijulikani ni mradi wa nani na wameingiza kiasi gani na matumizi ni nini.

Halafu leo unaambiwa hela ya michango ya ujenzi wa uwanja ilitumika kuweka uzio na matumizi ya kambi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom