rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 16,784
- 23,312
Naomba hii mada ijadiliwe na watu wenye uelewa. Moja ya taarifa kubwa inayojadiliwa ni usajili wa mchezaji Lawi kutoka timu ya Coastal kwenda Simba. Hii ni baada ya timu ya Coastal kupitia kwa msemaji wao kukanusha taarifa ya Simba kumsajili mchezaji wao wakati walishindwa kutimiza malipo kwa wakati.
Kwa mujibu wa kanuni za Bodi ya ligi na TFF kanuni no 75 kipengrle cha 4 kinaeleza mchezaji aliye na umri chini ya miaka 18 hatakiwi kupewa mkataba zaidi ya miaka 3. Aliyekuwa Mchezaji wa Coastal ametimiza miaka 18 mwaka huu na alikuwa na mkataba wa miaka 4 unaoisha mwaka 2025 hivyo kwa mujibu wa kanuni hii mkataba huo ulikuwa batili na kwa sababu mkataba ulikuwa batili Coastal hawakustahili kupewa hata senti tano.
Nimeambatanisha na kanuni hizo ili wale waliozoea kubisha wazisome