Simba hawastahili kuwalipa coastal hata senti tano

Simba hawastahili kuwalipa coastal hata senti tano

rodrick alexander

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Posts
16,784
Reaction score
23,312
Naomba hii mada ijadiliwe na watu wenye uelewa. Moja ya taarifa kubwa inayojadiliwa ni usajili wa mchezaji Lawi kutoka timu ya Coastal kwenda Simba. Hii ni baada ya timu ya Coastal kupitia kwa msemaji wao kukanusha taarifa ya Simba kumsajili mchezaji wao wakati walishindwa kutimiza malipo kwa wakati.

Kwa mujibu wa kanuni za Bodi ya ligi na TFF kanuni no 75 kipengrle cha 4 kinaeleza mchezaji aliye na umri chini ya miaka 18 hatakiwi kupewa mkataba zaidi ya miaka 3. Aliyekuwa Mchezaji wa Coastal ametimiza miaka 18 mwaka huu na alikuwa na mkataba wa miaka 4 unaoisha mwaka 2025 hivyo kwa mujibu wa kanuni hii mkataba huo ulikuwa batili na kwa sababu mkataba ulikuwa batili Coastal hawakustahili kupewa hata senti tano.

Nimeambatanisha na kanuni hizo ili wale waliozoea kubisha wazisome
 
Attachments

Coastal siwaelewi sijui wana bifu gani na Simba.

Hata kipindi tunamchukua Mgunda wali react hivi hivi kuwa wao bado wanamtambua Mgunda kama kocha wao.

Na kuna mchezaji mwingine pia kabla naye aliwahi kuletewa zengwe hivi hivi.
 
Ulivyoelezea utafikiri nyinyi(Simba) ndio mnahaki na huyo mchezaji.

Acheni janjajanja!
Soma kanuni usikimbilie kupinga, kanuni za usajili asilimia kubwa wamezicopy fifa au tafuta kanuni za fifa kuhusu usajili wa wachezaji chini ya miaka 18
 
Attachments

Kwa hiyo na nyinyi mnaamini kweli huyo Lameck Lawi ni U 20! Kisa tu amejisajili hivyo pale TFF!
 
Kwa hiyo na nyinyi mnaamini kweli huyo Lameck Lawi ni U 20! Kisa tu amejisajili hivyo pale TFF!
Passport yake inaonyesha umri wake ni miaka 18 lakini mkataba walioingia na coastal ni miaka 4 ambao unaisha mwaka 2025 na unapingana na kanuni za mikataba za TFF kuhusu usajili wa mchezaji wa umri wa chini ya miaka 18
 
Kwa hiyo kama huo umri wake unapingana na kanuni za TFF, ndiyo unawapa nyinyi simba haki ya kumsajili bila ridhaa ya timu inayommiliki huyo mchezaji?
 
upo sahii kikanuni. shida ipo kwenye usajili. tff portal kasajiriwa kama mchezaji wa coastal hapa ukilipa bado kama kwenye portal bado wa coastal ni wa coastal. so sign contract and not changing ownership. doesn't verify kama ni mchezaji wako.

swala la lawi simba hata waende wapi, bado atakuwa wa coastal despite both parties kuvunja sheria.
 
Tff ndio wametengeneza kanuni za mikataba, Kama kanuni hazikufatwa ni wazi mkataba ulikuwa batili, labda siasa zitumike Kama Singida black star walivyovunja kanuni za uhamisho wakapeleka wachezaji zaidi ya watano kwa uhamisho wa mkopo kwa timu moja.
Sheria na kanuni za mpira zimeigwa toka fifa hili swala likienda mbele litawaumbuanTFF
 
Sasa Simba walilpa pesa za nini kama ni hivyo?
 
Back
Top Bottom