Simba iachane na Kocha Pablo mapema

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,181
Reaction score
1,579
Nakubaliana kwamba huwezi uwe na ma-striker aina ya Boko, Kagere, na Mugaru, halafu tena utake kuchukua klabu bingwa au shirikisho. Huko ni kujenga gorofa wakati huna pesa.

Lakini hutafanya hivyo pia ukiwa na kocha ambae hajui hata kupanga kikosi chake kinachoanza. Namaanisha hana kikosi maalum cha mauaji.

Wala hajui kwamba huyu mchezaji sasa nimtoe, maana haisaidii timu, na makosa mengine kibao. Ndiposa nashauri kwamba Simba iachane naye kungali mapema.

Kwa maana huyu hata ubingwa wa ligi yetu ya wa-hapahapa hachukui, nini shirikisho.

Mwisho: Jamani mkitaka kuwa na mafanikio kwenye mashindano makubwa sajirini wachezaji wazuri, acheni kushobokea sana makocha wa ulaya.

Mbona kuna makocha wazuri wa ligi yetu ya wa-hapahapa wakikupangia kikosi huchomoki.

Haya jamani, msije kusema sikuwaambia!
 
Sisi tuna imani na timu yetu! Wachezaji wetu! Na kocha wetu Pablo. Wewe utakuwa umepewa tu bashasha ya kaki na Gii Esi Emu! Siyo bure.
 
Mimi ni simba siyo uto wa hapahapa.
Lakini tena huwa sina mapenzi upofu katika suala la mafanikio ya timu yangu.
Sisi tuna imani na timu yetu! Wachezaji wetu! Na kocha wetu Pablo. Wewe utakuwa umepewa tu bashasha ya kaki na Gii Esi Emu! Siyo bure.
 
Nitajie kocha mzawa anayeweza kufundisha simba.Ibenge au kocha wa al haily hawako pale kwa bahati mbaya bali uwezo na vyeti vyao. Pablo ana matatizo ila tatizo kubwa ni uongozi wa simba kutosajili wachezaji wazuri na kubaki na wachezaji mizigo
 
Nitajie kocha mzawa anayeweza kufundisha simba.Ibenge au kocha wa al haily hawako pale kwa bahati mbaya bali uwezo na vyeti vyao. Pablo ana matatizo ila tatizo kubwa ni uongozi wa simba kutosajili wachezaji wazuri na kubaki na wachezaji mizigo
Wataje hao mizigo
 
Jana Efue Morris alionesha uhai mkubwa sana kipindi cha pili. Pablo angemuanzisha kuanzia kipindi cha kwanza, huenda timu ingekuwa na uhai.

Mechi ya marudiano, mumshauri Pablo aachane na utaratibu wake wa kujaza wachezaji wazee uwanjani! Maana wanashindwa kabisha kunyumbulika. Mtu kama Erasto Nyoni, ifikie wakati astafishwe kwa manufaa ya timu.

Ni wakati sasa kwa vijana kama akina Jimmy Mwanuke, na wenzake kuaminiwa kwenye kikosi cha kwanza.
 
Mkuu Kumbe ukiwa hujavuta bangi zako huwa unaongea point?
 
Mkuu, wachezaji vijana wanatoka wapi Simba..? Timu Ina Wazee tu kuanzia kipa mpaka mshambuliaji..
Tujipange tu mwakani
 
mambo ya simba hayawahusu

Kwa nini hayatuhusu mkuu! Yanga itakuwa bora iwapo kutakuwepo na simba bora.

Ndiyo maana misimu miwili iliyopita, mlitusema sana kuhusu kikosi chetu dhaifu cha akina Yikpe na Sarpong! Tuliwasikiliza, na kufanyia kazi maneno yenu! na leo hii tuna Fiston Mayele Mzee wa kutetema!! Tuna dokta Aucho! Screen Protector! Na mastaa chungu nzima!

Na mwisho kabisa, timu inaendelea kufanya vizuri.
 
Lakini wakati mwingine tuangalie . Simba ina majeruhi wengi wa kikosi cha kwanza.
1. Lwanga
2.mkude
3.kibu
4.Lary bwalya
5.Mugalu
Ndiyo hivyo tena Chama hatumiki. Unategemea nini?

Kigezo cha Yanga kutolewa na Rivers huwa mnasema nikukosekana kwa aucho ,mayele na Djuma. Sasa kwa simba inakuwaje mnang'ang'ana na kejeli zisizo na Maana?
 
Wewe unatoa maoni kama mwanamichezo bila kujali timu unayoshabikia, hoja yangu iliwalenga wale waliotanguliza ushabiki badala ya kujadili mada husika
 
Kocha kama kocha nafasi yake ni kubwa ktk mafanikio uwanjani. Kwani yule aliyetimuliwa ndiye alisajili wachezaji waliopo? Mbona unaongea kama umekula choo yenyewe!
Kwani Pablo ndiye amewasajili hao wachezaji? Mbona unabwabwaja kama umekunywa maji ya chooni? Hao makocha wa ndani unaosema wanachoweza ni kupaki bus na kuumiza wachezaji wa timu pinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…