Simba ijitoe CAF Club Champions 2023/2024

Simba ijitoe CAF Club Champions 2023/2024

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Msimu ujao michuano mipya, ambayo ndio ya hadhi ya juu zaidi katika ngazi ya vilabu Africa Super League inaanza. Ujio wa mashindano hayo hautafuta CAF Club Championship ambayo kwa msimu huu Simba bado inashiriki na tayari imeingia robo fainali.

Michuano ya Africa Super League itajumuisha team 8 ambazo zote zitapambana home and away. Hivyo Simba mwakani itacheza mechi 14 ngumu za Africa Super League. Simba kwa msimamo wa NBC league inayoendelea sasa hivi ni dhahiri ita qualify kushiriki CAF Club Championship msimu ujao, na kama itafika robo fainali (Ni kawaida yao kwa sasa hivi) msimu ujao itacheza mechi 12.

NBC League TZ Simba inacheza mechi 30. Azam Confederation Cup angalau mechi 5, Mapinduzi Cup angalau mechi 3. Hapo utaona mwakani Simba itapaswa kucheza mechi za mashindano angalau 61, sijajumuisha pre season, mechi za kirafiki na Simba day. Hapo tukumbuke karibu Ist eleven yote ya team Wana majukumu ya kuchezea team za mataifa yao katika mechi za mashindano na kirafiki, na mwakani February Kuna Afcon.

Ili Simba iweze kufsnya vizuri Africa Super League, na kwa afya nzuri ya wachezaji ikiwemo kupunguza injuries nashauri Simba ijitoe CAF Club Championship msimu ujao. Vinginevyo iruhusiwe kusajili kikosi kipana cha wachezaji 40, na foreigners waongezwe wafike 18, na Simba itumie fursa hiyo kusajili wachezaji wa viwango kweli kweli, sio akina Quattar.
 
Pauln na siyo Paulin, Sina undugu na Teja
 
Kwahiyo na wengine wajitoe au simba tu
Ndio maana katika thread yangu mwishoni nimetoa alternative (Plan B) waruhusiwe kusajili wachezaji 40, wakiwemo 18 foreigners.
 
Simba ina kikosi kipana. Hivyo watagawa wachezaji, na makombe yote wataendelea kuyachukua. Kuanzia kombe la robo fainali klabu bingwa, mpaka lile la mapinfuzi.
 
Msimu ujao michuano mipya, ambayo ndio ya hadhi ya juu zaidi katika ngazi ya vilabu Africa Super League inaanza. Ujio wa mashindano hayo hautafuta CAF Club Championship ambayo kwa msimu huu Simba bado inashiriki na tayari imeingia robo fainali...
Huyo Outtara ana shinda gani na wewe au amekuchukulia demu wako?
 
Back
Top Bottom