Nimeangalia gemu ya Simba vs Al Hilal na nimebaini yafuatayo.
1. Simba ina uwezo kwa sasa kucheza na timu yoyote duniani bila kumtegemea Manula wala Benno, hili jambi Utopolo hawawezi kuthubutu
2. Pamoja na shutuma, matusi na kebehi kwa uongozi wa Simba kuhusu usajili, Simba wamewekeza sana kwenye pitch kuliko nje ya uwanja kama utopolo
3.Kikosi kilichocheza na Al Hilal kilitushtua wengi, lakini kimedhihirisha kuwa mpira ni mbinu na mfumo.
4.Katika modern football sio lazima uwe na viungo wakabaji ndio ucheze vizuri, Kocha wa Simba amethibitisha hilo.
5.Modern football inataka mchezaji awe na uwezo wa kucheza namba yoyote uwanjani, Zoran Mack ametuonyesha Leo kwa Peter Banda, Chama na Mwinuke
6.Zoran Mack ametuonyesha namna gemu za ugenini zinavyopaswa kuchezwa kwa adabu, Al Hilal ya Ibenge sio ya kawaida kama tunavyodhani
7.Kama Simba imecheza na wachezaji kama Salim, Mwinuke, Gadiel, Israel, Kapama ambao hawapo first eleven, itakuwaje kikosi kikikamilika
8.Kwa namna Simba wanavyosambaza upendo uwanjani kwa pasi milioni 1, nimeamini wanapocheza na utopolo kuna hujuma zinafanywa na watu ndani ya timu yetu ili tupoteze.
9.Simba ikipata striker wa maana hakuna wa kupata sare
10.Simba hii ikishinda nyumbani bao 3 0 na ugenini ikacheza hivi kama ilivyocheza Leo na Al Hilal, am sure inakwenda kucheza final
11.Simba nguvu moja, wale wanaotaka madaraka katika uongozi wasubiri kwanza, kuuza gemu kwa utopolo ni ufala wa kiwango cha chuo kikuu
12.Simba msisikilize waandishi wa michongo, tuendelee kuleta heshima katika nchi hii kwani utopolo kuhangaika kwao kutaishia kwa Al Hilal
NB Hongera sana Zoran Mack, Bila Kanoute wala Mkude wala Akpa lkn shughuli imeonekana pale Sudan.