Simba imeenda kuutumia uwanja wa Jamhuri bila kuujaribu

Simba imeenda kuutumia uwanja wa Jamhuri bila kuujaribu

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Hii timu kimya kimya bila mbwembwe niliacha kuiangalia, nafuatilia tu matokeo yake kutokana na kwamba kuna upuuzi mwingi sana ambao lawama zote zinaangukia katika uongozi.

Simba iliuchagua uwanja wa Jamhuri Morogoro kama uwanja wake wa nyumbani ila cha kushangaza, wachezaji wa Simba wameenda kwenye mechi ya leo dhidi ya Prisons huku wakiwa hawajafanya mazoezi kabisa katika uwanja huo. Timu kubwa itafanyaje kosa kubwa la kiufundi kama hilo?

Baada ya kuwatesa vya kutosha mashabiki wa Dar es Salaam hadi mpaka leo wengi sana wameikatia timu tamaa, sasa uongozi umeamua kuwapelekea uchungu mashabiki wa Simba wa mikoani. Sababu ya kuukimbia Chamazi siyo ishu za kuhujumiwa kama wanavyodai, ni kwa sababu mashabiki wa Dar hawana mwamko sana na hii timu kwa sasa. Bado huko mikoani unaweza kuwaokota okota wakajaza uwanja ila.....

Tukiendelea hivi, na hao wa mikoani nao watakata tamaa na hii timu na baada ya miaka 2 Simba itakuwa timu ya kawaida sana katika ligi.
 
Ni ya kawaida mpaka ikifungwa 5 yanalipiwa mabango na kuku zinapikwa na chapati.
Kiredio anakushangaa
 
Attachments

  • FB_IMG_17097394475222637.jpg
    FB_IMG_17097394475222637.jpg
    144.6 KB · Views: 5
Ni ya kawaida mpaka ikifungwa 5 yanalipiwa mabango na kuku zinapikwa na chapati.
Wakati mwingine weka ushabiki pembeni uangalie vitu kwa uhalisia. Niliwahi kusema viongozi wa Simba wamejipa mamlaka ya kuamua lini wanasimba wawe na furaha na lini wahuzunike. Ndiyo tunachokiona msimu huu.
 
Kwanin hawakufanya mazoezi kwenye uwanja huo
 
Watu wa mpira hatukurupuki.

Kuna mdau mmoja wa mpira tena Yanga lialia Tate Mkuu aliwahi kukiri kuwa kuinyima timu pinzani fursa ya kufanya mazoezi ni mbinu nzuri ya kisaikolojia kuivuruga timu hiyo.

Sheria inawataka siku moja kabla ndiyo wafanye mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kwa ajili ya mechi.

Nawapongeza wadau wote waliowafanyia hiyo hujuma ya kuwanyima uwanja wa mazoezi. Kwa hapa tulipofikia, siyo mbaya kumharibu kisaikolojia mpinzania wako, kupitia vitu vidogo kama hivi.
 
Watu wa mpira hatukurupuki.

Kuna mdau mmoja wa mpira tena Yanga lialia Tate Mkuu aliwahi kukiri kuwa kuinyima timu pinzani fursa ya kufanya mazoezi ni mbinu nzuri ya kisaikolojia kuivuruga timu hiyo.
Comrade mbona umeyachukua maneno kutoka kwenye uzi ambao siufahamu na kuniwekea hapa? Halafu hata kama niliandika mimi, bado hoja iko pale pale!

Hiyo ni mbinu ya kuwekewa zengwe kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo, bado haitoi kibali cha kususia mechi! Huu ni utoto.
 
Hayo mazengwe hayakubaliki katika mpira na ndiyo tupo hapa tunayapinga. Ikiachwa kila mtu ajiamulie anavyotaka hautakuwa tena mpira.
 
Back
Top Bottom