NG'OTIMBEBEDZU
JF-Expert Member
- Aug 11, 2010
- 1,180
- 595
Babu Onyango, Usajili ni kama kucheza kamali. unaweza kupata au ukakosa, ukifuatilia sajili za nyuma utakubaliana na mimi. Ndiyo maana mimi binafsi huwa nasubiria kuona matunda ya usajili.Hata mzungu, okwa, akpan,kapama Kibu d kyombo wote tulisema na wamefloo wote
Mpira tunauangalia kwa macho tofauti. Mpira wetu umetawaliwa na vitu vingi sana, kuna kukurupuka, yaani unakurupuka kusajili mchezaji hata huna mipango naye mradi tu umemuona kafanya vizuri kwenye timu X.
Kuna kubania yaani unasajili mchezaji hata kama hukumtaka kwa hofu tu huyu akienda timu nyingine watafaidi.
kuna udhaifu mkubwa sana kwenye technical teams kwenye vilabu vyetu sababu unasajili mchezaji bila hata kumfuatilia kwamba huyu ataendana na pressure ya timu yetu!
Kuna usajili wa kuridhisha tu mashabiki ambao wameangalia clips za mchezaji kwenye U -tube, hata kama ni za mwaka 2001 wakadhani kuwa 2022/23 mchezaji atakuwa vilevile.
Mchezaji anaweza akawa mzuri lakini asifiti kwenye timu kwa sababu mbalimbali ikiwepo kutoelewana na wenzake sababu ya inferiority complex za wenyeji aliowakuta, au kocha akaiogopa profile ya mchezaji akashindwa kuendana naye, au mchezaji anafika kwenye timu anakutana na mazingira tofauti na kile kilichokuwa stated kwenye contract agreements au "manbo yetu ya kiswahili" (hii anajua zaidi Mecky Mexime mimi siwezi kuizungumzia sana).
Kwa hiyo, mara nyingi sisi huwa tunafanya "players recruitment" na si usajili katika maana ya kuimarisha timu.