Simba imesonga mbele baada kuifunga Gendarmerie goli 1 kwa bila

m2kutu

Senior Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
125
Reaction score
101
Wasalaam wadau wa sports, ningependa kujua mechi ya marudiano kati ya Gendarmerie na Simba Sc itaonyeshwa live kupitia channel gani kwan Azam tv wamesema hatoweza kuirusha hii mechi.

Natanguliza shukran zangu kwenu wadau.

UPDATES

Simba imesonga mbele katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuifunga Gendarmerie bao 1-0, ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 5-0.

Klabu ya Simba Sc,imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Gendarmerie ya Djibout, katika mchezo wa marudiano.

Simba imefanikiwa kupata bao hilo kupitia mshambuluaji wake Mganda Emmanuel Okwi kwenye dakika ya 55 ya kipindi cha pili.

Kwa matokeo hayo Simba inafuzu katika hatua hii ya awali kombe la Shirikisho barani Afrika kwa jumla ya bao 5-0.

Katika mchezo wa awali uliofanyika hapa chini katika dimba la Taifa-Jijini Dar es salaam, Simba walifanikiwa kupata ushindi wa bao 4-0.

Baada ya matokeo hayo Simba itakutana na Al-Masry ya Misri iliyopokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Green Buffaloes.

Pamoja na kufungwa bao 2-1 Al- Masry ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 4-0 katika mchezo wa awali na kufanikiwa kusonga mbele kwa jumla yabao 5-2.

Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yussuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, James Kotei, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi na Muzamil Yassin
 
Naweka kigoda changu hapa,

Asikitoe mtu kesho ntakikuta.
 
Wasalaam wadau wa sports, ningependa kujua mechi ya marudiano kati ya Gendarmerie na Simba Sc itaonyeshwa live kupitia channel gani kwan Azam tv wamesema hatoweza kuirusha hii mechi.

Natanguliza shukran zangu kwenu wadau.
Kama Azam WAMESHINDWA SUBIRIA ABOOD TV MKUU HOPE WATAKULETEA PAMBANO LIVE
 
Kwa jinsi nilivosearch mtandaoni, nimegundua kuwa mechi ya gendarmerie vs Simba haitoonyeshwa na channel yoyote ile iwe Tanzania au Djibouti.

Hii inatokana na nchi mwenyeji kuwa na muamko hafifu wa mchezo wa soka na pia hawana technology ya kutosha kuweza kurusha mechi hii. Kwa mfano hiyo channel ya taifa iitwayo RTD tv ambayo ndo ilikuwa tegemeo kubwa la wadau wengi kuwa wangerusha hii gemu ni ya hovyo sana bora hata TBC 1.

Hivyo wadau tufuatilie tu matokeo kupitia live scores tu, kuhusu mdau aliesema tusubiri ABOOD tv pia atakuwa amefeli kwa sababu na wao wanategemea wapate mawasiliano kutoka channel za Djibouti.

Ni hayo tu wadau wa sports..
 
Wasalaam wadau wa sports, ningependa kujua mechi ya marudiano kati ya Gendarmerie na Simba Sc itaonyeshwa live kupitia channel gani kwan Azam tv wamesema hatoweza kuirusha hii mechi.

Natanguliza shukran zangu kwenu wadau.
TBC taifa hawatangazi?
 
Jaman nauliza anaejua channel gan wanaonesha hii game ya leo ya simba anijuze tafadhar
 
Nikadhani supersport wangerusha,kumbe haka kafurushi kangu ka bomba kanarusha mechi zingine tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…