kingphisher
Member
- Nov 30, 2024
- 45
- 79
Yaani mmekuwa na muda wa takribani wiki moja ya kufanya mazoezi na maandalizi yenu yote, mmetumia gharama kubwa sana halafu mnasusa mechi kisa kunyimwa kufanya mazoezi usiku?
Simba mpo sahihi kusikilizwa, lakini si haileti tija kususa mchezo.
Kususa mchezo ni sawa na kujichukulia sheria mkononi.
Nyie mngecheza hafu tff ije itoe adhabu kwa wenyeji wa mchezo.
Kwa akili ya kawaida, timu haijasafiri kutoka nchi nyingine wala mkoa mwingine hadi dar, unadai mnasusa mchezo kisa tu hamjafanya mazoezi kwa siku moja, kwa uchovu ghani hadi mshindwe kucheza mechi kisa hamjafanya mazoezi?
Hapa simaanishi waliochukua maamuzi wa kuwazuia wapo sahihi, hapana. Ni kwamba, taarifa zimeenea mtandaoni, na tff na bodi ya ligi wameona.
Hiyo sio sababu ya kususa mechi, badala yake simba wangecheza then baadaye ndo wafatilie haki zao kwa nini wakatazwe kufanya mazoezi, tff na bodi ya ligi watachukua hatua za kisheria.
Kilichopo ni kwamba, ikitokea simba wamesusa mchezo, yanga wataenda uwanjani na watapewa point tatu na magoli matatu.
Kutokufanya zoezi haiwezi kuwa sababu ya kususia mchezo bhana.