Simba ina mashabiki "passionate" wenye hisia na timu yao

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Ndiyo, adhabu ambayo CAF wameipiga Simba ikiwepo ya pesa na kutoingiza mashabiki inauma na hakuna mwanasimba aliyeifurahia.

Ni muhimu tukakumbuka kuwa Simba si timu ya kwanza kupewa adhabu hiyo. Wydad, Al Ahly, Esperance na USMA, ni miamba wengine wa Africa wamewahi kupewa adhabu ya namna hiyo. Huko Ulaya pia Bayern Munich, PSV na vilabu vingine vikubwa vimewahi kukumbwa na adhabu hii, tena zaidi ya mara moja. Huko Ugiriki mechi za ligi nzima zilichezwa kwa muda bila mashabiki. Hili siyo jambo geni.

Duniani kote timu zinaombea zipate "passionate fans" au "mashabiki wenye hisia". Mashabiki hawa wanakuja viwanjani kwa wingi, wanashangilia na kuipa morali timu yao kwa hali na mali. Simba imekuwa na sifa ya kuwa na mashabiki hao.

Waangalie Azam FC wana pesa, wana kikosi kizuri ila hawana "passionate fans". Nenda kule Mamelodi, pamoja na mafanikio yao ila ni hivyo hivyo hadi wanatoa tiketi bure hata katika mechi zao kubwa. Hapa Tanzania kuna katimu kanaitwa Yanga sijui, mashabiki wake ni wa kununuliwa supu na kupewa tiketi za bure waende uwanjani maana hawana "passionate fans". Hizi timu zote nilizotolea mfano ukiwaambia unawapa mashabiki wa Simba hata kwa siku moja tu, watatoa meno yote 32 nje kwa furaha na vigelegele.

Soma Pia: Klabu ya Simba imefungiwa na CAF kucheza bila mashabiki na faini zaidi ya TSh. Milioni 100

Ndiyo, vurugu katika michezo siyo nzuri na siziungi mkono. Simba haina historia ya kufanya vurugu katika michezo. Simba siyo Abajalo ya Sinza. Hauwezi kucontrol hisia za watu 40,000 hasa waliochochewa kuonyesha hisia hasi. Timu ya Sfaxien ilichochea vurugu na hadi kuwapiga watendaji wa uwanja. Ukiangalia video za tukio kwa jicho la kiuchunguzi utagundua Sfaxien walikuwa wanachochea vurugu. Watendaji wa uwanja nao walionyesha weledi mdogo katika tukio zima na hapo sijaongelea uwanja kutokuwa na uwezo wa kuwabaini wahusika ambao wengine wanaweza kuwa ni mamluki waliotumwa kuharibu sifa ya Simba.

Hata hivyo ukiacha chanzo na wahusika wa tukio, kama yalivyo maisha, wakati mwingine dharau zikizidi inabidi umkumbushe mtu heshima unayostahili. Siku nyingine mashabiki wa nje wakija kucheza na Simba, kuna kaadabu fulani katakuwepo.

Narudia tena, siungi mkono vurugu ila pia siungi mkono kuwa timu ya mafala ambapo timu na watu wanaweza kuichukulia poa. Ukionekana dhaifu, jiandae kufanywa chochote na yoyote. Simba ikemee vurugu viwanjani ila pia isikubali kujulikana kama timu ya kuchukuliwa poa.

Heshima haiombwi inachukuliwa.
 
Tumshukuru Mwamedi kwa kuwekeza kuwatubini wapinzani wake kwa njia mbalimbali wakiwemo Marefa, Makocha na baadhi ya wachezaji.

Ndio maana haitatokea mchezajo kitoka Simba kusajiliwa kwenye timu maarufu nje ya Tanzania kuweza kuwika sababu sio ubora wa mchezaji bali ni ngawira zinazotenbezwa na Mwamedi!
 
Endelea kujifariji,makolo au madunduka mmezoea kuvunja viti viwanjani Wala siyo mara ya kwanza.
 
Tumshikiru Mwamedi kwa kuwekeza kuwatubini wapinzani wake kwa njia mbalimbali wakiwemo Marefa, Makocha na baadhi ya wachezaji.

Ndio maana haitatokea mchezajo kitoka Simba kusajiliwa kwenye timu maarufu nje ya Tanzania kuweza kuwika sababu sio ubora wa mchezaji bali ni ngawira zinazotenbezwa na Mwamedi!
We jamaa kituko samata alitokea huko utopoloni?
 
Duniani kote timu zinaombea zipate "passionate fans" au "mashabiki wenye hisia". Mashabiki hawa wanakuja viwanjani kwa wingi, wanashangilia na kuipa morali timu yao kwa hali na mali. Simba imekuwa na sifa ya kuwa na mashabiki hao.
Wewe kweli kolo acha kutetea ujinga. Kuwa shabiki passionate sio lazima kuvunja viti. Huo ni uzwazwa na nyie ndio mnaoingia kwenye mechi nyingine mnafanya huo uzwazwa wanaadhibiwa wengine shenzi kabisa.

Nawaonya hiyo tabia ikome na muache mara moja.
 
Lipeni faini, na achaneni na tabia ya kuukumbatia ujinga na umbumbumbu. Kila siku nyinyi ni kung'oa tu viti vya uwanja wetu wetu wa Taifa!
 
Tumshikiru Mwamedi kwa kuwekeza kuwatubini wapinzani wake kwa njia mbalimbali wakiwemo Marefa, Makocha na baadhi ya wachezaji.

Ndio maana haitatokea mchezajo kitoka Simba kusajiliwa kwenye timu maarufu nje ya Tanzania kuweza kuwika sababu sio ubora wa mchezaji bali ni ngawira zinazotenbezwa na Mwamedi!
Deluded
 
Wewe kweli kolo acha kutetea ujinga. Kuwa shabiki passionate sio lazima kuvunja viti. Huo ni uzwazwa na nyie ndio mnaoingia kwenye mechi nyingine mnafanya huo uzwazwa wanaadhibiwa wengine shenzi kabisa.

Nawaonya hiyo tabia ikome na muache mara moja.
Lakini,vyura mmepewa supu na mahindi ya kuchoma ili mpate nguvu za kushangilia.
NB;Bado pointi ngapi na ninyi vyura muitwe "Mwakarobo"!
 
Sijui kwa upande wenu nyie wengine... Ila kwa huku niliko sijawah ona shabiki wa Simba mwenye akili timamu. Walah umbumbu na ushabiki wa Simba ni pete na Kidole. Ovaa
 
Back
Top Bottom