Simba ina mengi ya kujifunza kwa Petro de Luanda

Simba ina mengi ya kujifunza kwa Petro de Luanda

Kupaki bas ni mbinu ya mpira. Na usidhani ni kitu kepesi hivyo kupaki bas na kufaulu kusonga mbele. Uliza Simba wamechezesha walinzi karibia saba lakini kashindwa ugenini kutoboa
Jifunze kufatilia kitu kabla haujaamua kujiingiza, jamaa alisema kuwa Petroleos hawapaki basi ugenini kwahiyo nilikuwa namuelekeza mechi ambazo petro walipaki basi. Hakuna sehemu ambayo nimekataa kuwa kupaki basi sio sehemu ya mchezo.

Mbinu ya Simba Sc kujilinda ilifanikiwa na ndiomaana walitoka kwa penalty.
 
Watu mnajua kukuza mambo madogo yanekane makubwa[emoji23], ni kweli wamesajili kwa hela ndefu ula hilo swala la 22B kadanganye kwenye magenge ya kahawa.
Nidanganye nipate nini nenda transfer market ukaone value ya wachezaji wao mchezaji atoke ligi kuu Portugal utamlipa million 10?
 
Hawa jamaa wanacheza kama wako kwao.
Jamaa wana timu nzuri na wachezaji hawakosei pass wala kushindwa kujiamini.
Unatazama soka mpaka unafurahia.
Tuna mengi sana kujifunza kwa nia nzuri tu!
Uliangalia first leg kwao Angola? Walicheza kinyume na ulivyochambua hapo. Mi naona hawajielewi, yaani wanashindwa kujua wafanye nn? sehemu gani?

Unafungwaje nyumbani goli 3 kisha unataka ukashinde away goli Zaid ya 2 ili ufuzu? Aliwezaga Simba tu dhidi ya team moja ya Zambia(nimesahau jina) alifungwa 4-0 shamba la Bibi Kisha akaenda mpiga mtu 5-0 kwao.
 
Kwahiyo tuseme timu nyingine mmesalimu amri? Mmeamua kuwaachia simba msala wa kulipaisha soka la TZ?

Kwanini usiseme vilabu vya Tz viwaige petro atletico wewe unawataja tu simba? Au tuseme Yanga wao tayari wamesharidhika na Hali yao kwamba wao niwawazee wa nje ndani?
 
Yanga ni zaidi ya Petro Atletico.
 
Kwahiyo unataka kusema kuwa Petroleos hawakupaki basi kule SA? We jamaa bwana😀
Unajuwa kila mechi unaikabili tofauti ile na Sundown walikuwa wameshinda kwao ilikuwa ni kutafuta draw hata walipofungwa moja wakabadilika kutafuta goal wakarudisha mechi ya jana walikuwa wako nyuma ya goal 3-1 kwa hiyo walikuwa wanatafuta ushindi ila ni team nzuri sana na team nzuri ni pale unapoikabili game kutokana na mahitaji ya mechi kwa maana wanaweza ku park bus na wanaweza kuachia bus. Tukirudi kwenye mada ni kweli team zetu wawakilishi mwakani kama hatutajipanga basi tutaishia kucheza confederation. Kuna gap kubwa na team za champions league kule ndio pakucheza kwa miamba na ndiko pakujifunza kama tunataka kuwa wakubwa barani Africa. Yanga na Simba ni lazima wapate wachezaji wa kuweza kucheza mashindano haya japo Simba marekebisho yake inaweza ikawa sio makubwa sana anaweza kuongeza wachezaji wa 4 lakini bora sana ila kwa Yanga wanahitaji wachezaji wazoefu kwenye mashindano haya sio kwa ubaya ila Yanga wasijaze tu wachezaji ila wawe na quality kama wachezaji 6 mpaka 5. Simba yuko mbele ya Yanga kidogo sababu wamejifunza huko Yanga hajapata good run na mwaka jana walionesha udhaifu mkubwa. Juhudi kubwa za kuchukuwa ubingwa wanaweza kuondoka kwenye round ya kwanza tu investment yote ikawa kama bure tu.
 
Nidanganye nipate nini nenda transfer market ukaone value ya wachezaji wao mchezaji atoke ligi kuu Portugal utamlipa million 10?
Naelewa mkuu na sio kwamba sijui kuwa wamefanya usajili wa nguvu, nilichokataa ni 22B. Wamefanya usajili wa aoproximately 16B.
 
Hawa jamaa wanacheza kama wako kwao.
Jamaa wana timu nzuri na wachezaji hawakosei pass wala kushindwa kujiamini.
Unatazama soka mpaka unafurahia.
Tuna mengi sana kujifunza kwa nia nzuri tu!
Upo sahihi jamaa wamenifurahisha na hii performance yao ya away. Hivyo ndivyo unapaswa kucheza ukiwa away....weka ball down ngoma ipigwe sio unapaki treni alafu unategemea kupita. Semi final ya kibabe
 
Uliangalia first leg kwao Angola? Walicheza kinyume na ulivyochambua hapo. Mi naona hawajielewi, yaani wanashindwa kujua wafanye nn? sehemu gani?

Unafungwaje nyumbani goli 3 kisha unataka ukashinde away goli Zaid ya 2 ili ufuzu? Aliwezaga Simba tu dhidi ya team moja ya Zambia(nimesahau jina) alifungwa 4-0 shamba la Bibi Kisha akaenda mpiga mtu 5-0 kwao.
Mufurlira wonders mwaka 1974
 
Useme na Utopolo wakijifunze wapi?
 
Yanga ni zaidi ya Petro Atletico.
Uko sahihi mkuu. Yanga ni zaidi ya petro Atletico kwakuwa wao Wana sifa ya kipekee ambayo vilabu vingine hawana ktk ukanda huu wa Afrika ya kupigwa nje - ndani kila wanapoweka pua zao kwenye mashindano ya CAF na ushahidi upo wa kutosha Rivers utd ya Nigeria na pyramid ya Misri.
 
Wafuzu kuelekea wapi? Walishabugizwa goli tatu kule kwao, hakukuwa na mantiki ya wao kupaki basi na wakati wanahitaji kutafuta magoli(hata kama wako ugenini). Sasa wapaki basi ili iweje sasa.

Nenda kaangalie mechi yao na Mamelod kule SA jinsi walivyopaki basi.
Hata mechi ya kwanza walicheza utopolo tu
 
Mleta mada umesema kweli.
Simba ndo timu yenye uchu wa mafanikio makubwa kwa hapa Tanzania ni vema wakajifunza mambo mengi kwa waliotangulia kuanzia uwekezaji wa fedha mpaka benchi la ufundi.
Huwezi kuwa na uchu afu unakuwa na wachezaji wa hovyo ie Kagere, Mugalu ,Bocco, Wawa, Banda, Nyoni
 
Back
Top Bottom