DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Leo nimeona niiongelee kidogo timu yangu ya zamani, Simba SC.
Kwa hizi sajili, acha, sajili zinazofanyika kila msimu inaonyesha wazi Simba imepoteza kabisa kujiamini. Viongozi hawajui Simba inataka nini hasa na badala yake wanasajili na kuacha wachezaji tu ili waonekane wamefanya. Wachezaji kama Morris Abraham au Sowah siyo wa kuja kuikomboa Simba bali ni kuwaridhisha tu wanasimba ambao nao hawajui hata wanataka nini ila kwa kuwa wamewaona wanaona wachezaji wazuri.
Viongozi na mashabiki wa Simba wote wamepoteza kujiamini, hivi sasa timu inasajili tu ili kuondoa lawama.
Hauwezi kuwa mtu makini kwa kuwaacha kina Mavambo na Okejepha halafu unaenda kusajili sijui yule mwarabu wa Mombasa au yule Kantè ambao hawawazidi kiuwezo wale unaowaacha na pia wanaweza kuhitaji msimu mzima kuzoea ligi na mikikimikii ya mashindano ya ndani na nje, halafu baadae wakishazoea unawaacha. Wakati huo huo unabaki na Mutale na Kibu au kwa kuwa hawauziki?
Labda watuambie wameamua kuwa academy.