Nadhani mnaona siasa zinazoendelea huko mipirani.
Mara Sowah aliye na mkataba na Singida ameachiliwa BURE na Singida kwenda Simba kwa sababu eti Dewji kaongea vizuri na Mwigulu. Mara Feisal kakubali kila kitu, wakati huo huo Azam hawajakubali kumuuza (hivi kabla haujaongea na mchezaji, si inabidi kwanza klabu iridhie?).
Mipira umeingiliwa na masiasa. Kwa uzoefu wangu, ukiona drama za siasa zinakuwa nyingi kwa wakati mmoja, jua kuna jambo serious sana la kinchi linapitishwa kimya kimya au linafunikwa.
Poleni sana watanzania wenzangu.