Simba ipo kibiashara na upigaji, ndo maana viongozi hawataki kujiuzulu

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Tukisema Magungu na Try Again ni wapigaji watu wanasema tunawaonea.

Hadi leo hakuna mchangunuo wa hela waliyochangisha mashabiki kwa ajili ya uwanja. Haieleweki uwanja umeisha na hakuna feedback.

Mo ni mwekezaji mjanja matangazo mengi kwenye jezi,haijulikani yale matangazo kama analipia, Imagine mbet kwa tangazo moja wanalipia almost bil 5, yeye ana matangazo karibia 4 kwenye jezi, hiyo ina maana ile bil 20 aliyoweka kama ni kweli kairudisha kwenye matangazo na faida juu,sasa kaweka nini?

Hayo yote yanapitishwa na Magungu,Try Again na Kajuni, ndo maana Babra alikuwa akiongea kwa mafumbo akajiuzulu maana anajua upigaji.

Hakuna wachezaji wa maana wanaongeza tu sifuri kwenye kununua ndo maana unaona haya matokeo. Watu wamepiga kelele misimu iliyopita kuhusu Matola mzee wa kula 20 percent kwa wachezaji wa ndani now wamemrudisha sahau kama kina Bocco wataachwa.

Hela za bahati nasibu ya Shabiki Bingwa na Mfalme bingwa hakuna mchanganuo watu wanaunda tu kitu na kupitisha hakuna hata kwenye agenda za vikao halafu wanapiga pesa hamna usajili wa maana, hizo hela zinafanyiwa nini? Magungu akipata chake wakigawana kila mtu anakula bati,zinabuniwa tu mbinu za upigaji.

Wamedharau ligi kwa vile haina hela ikija michezo ya kimataifa macho yote pale watajikakamua ili wapige mgawo wa CAF na hata kama Mudy alisusia basi ataanza tena kama anajituma vile,hizo hela hamna feedback,hufanyi usajili wa maana na umekula mabilion ya club bingwa na African football league.

Mechi inapokuja iwe ya ndani au kimataifa Simba wataweka juhudi kwenye promo ili mashabiki wajitokeze wapige hela ya viingilio, misimu 5 simba inajaza uwanja na hakuna siku wameingiza mashabiki bure ila hakuna usajili wa maana hela zinaenda wapi?

Hawana mtu wa maana kwenye scouting, wamemweka mzungu wanasema ni professional matata sana, ukifuatilia hana historia ni shabiki tu wa Simba ambaye ana biashara zake za kilimo Mbeya na Iringa.

Tuanze na viongozi tusilaumu wachezaji .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora turudi zetu tena kwa Mangungu...ndiyo, hatumtaki Mangungu.
 
Wajiuzulu..? Waende Wapi?

Michanganuo hiyo Unataka wakupe Wewe...?

Nenda Kwenye Mikutano mikuu ya Klabu,huwa wanatoa Michanganuo..!


Ila hapo Kwenye Mashabiki kujaza Uwanja,ni Kweli Mashabiki Wa Simba Hawana Jambo Dogo....CAF Hawakukosea kuwapa tuzo ya Mashabiki Bora Afrika...!

Wala Hawahitaji Kuingizwa Bure Uwanjani na Boss...! Eti GSM day..!

Huyu mzee Gharib anajuta kuwafahamu UTO mnamkausha Damu...!Amlipe Aziz...hlf haitoshi Ailipie na Mishabiki inayopenda kitonga...AIBU..

Nipo paleeee...
 
Reactions: Tui
Oyaa kwahiyo mnasema superstar Onana sio chezaji la maana tena auu
 
Aliebuni msemo wa bado haujasema kumbe alikulenga wewe mkuu
 
Simba inayo matatizo makubwa sana yanayoanzia kwa mwekezaji mwenyewe, viongozi na wachezaji, Tunajua mbinu za wahindi uwa wanatumia Divide and rule ya wajerumani ili kufanikisha mambo yao ndicho anachofanya Mo, kaweka viongozi pale matokeo yanapokuwa mabaya yeye anajitoa anajificha kabisa anawatupia zigo kina mangungu na try again wapambane na wanachama, yanapokuwa mazuri utamuona anaibuka na tweet nyingi kwenye mitandao na kujitokeza hadharani aonekane yeye ndiye kafanikisha ushindi!
Simba msipoangalia uyu mhindi ni kirusi namba 1 ndani ya timu, alitumia nguvu nyingi kuendesha mchakato wa kupewa timu haraka haraka matokeo yake wanachama bila kujitambua Wala kujielewa wakapitisha katiba ambayo aziendani na matakwa ya kikanuni na Sheria za uwekezaji na mchakato ukazuiliwa na serikali wakaambiwa warudi wafanye marekebisho ya katiba waliyoipitisha aikuwa sawa!
Sasa uyu bwana Anakuwa anasema eti Kuna watu wanamkwamisha wakati yeye mwenyewe na janja zake ndiye anayejikwamisha!!
Aliwaweka kina mangungu ambae alikuwa ameshindwa uchaguzi ili kusudi walinde maslahi yake na yule karuwa aliyekuwa ameshinda alijua kabisa atoweza kumburuza kikondoo kondoo kura zikapinduliwa mangungu akarudi!
Kwa maana iyo akuna Cha maana anachoweza kumhoji mwekezaji aliyefanikisha urejeo wake kwenye uongozi, atakuwa ni kiongozi wa ndiyo Mzee kwenye Kila kitu yeye na Try again!
Unaporudi uku kwa wanachama na wao wamegawanyika tiyali effect ya mhindi kuwagawanya na kuwatawala ishafanya kazi, Kuna wanachama wanaojua kabisa kuwa mhindi ni tapeli na awamuungi mkono ata kidogo wale ni wanaojitambua wanaojua kinachoendelea klabuni, alafu Kuna kundi jingine la wanachama ambao wao wananufaika na uongozi uliopo, wanapewa tenda za kuuza jezi na viongozi uko mitaani na wengine wanavuta mpunga kutoka kwa viongozi ili wawapigie debe uko kwa wanachama wawaunge mkono, wale ndio mnaowaona kina kisugu, mzaramo, mwakitalima, na wenzake,
Kuna kundi jingine la Wanachama ambao wao ni bendera fuata upepo, wanaangalia matokeo ya timu uwanjani basi, yakiwa mabaya wanamrudia mangungu, yakiwa mazuri wanamsahau mangungu wanamshukuru Mo kwa kuitengeneza timu🤣🤣🤣!!!
Kwa stahili hii Simba inayo kazi ya ziada kurudi kwenye njia yake maana mhindi keshawavuruga vya kutosha wakati huo aijulikani Ile b.20 aliiweka kwenye account Gani!
 
Thread inahusu Simba usitoke kwenye mstari
 
Umeongea ukweli ambao wengi wanaijua Ila hawataki kuusema, mo ndiye kirusi namba moja, rekodi ya mo kuongoza timu inatia shaka toka mbagala market Hadi singida United. Mo alitumia pesa nyingi kuharibu mchakato wa uwekezaji, kwanza alitengeneza mazingira ya yeye kuwa mwekezaji pekee kwa kutoa misaada na mikopo kablamchakato haujaanza. Wakati Sheria inasema uwepo wa wawekezaji wasiopungua watatu yeye kwa kutumia pesa na ushawishi alihakikisha anakuwa mwekezaji pekee Tena mwenye nguvu zaidi ya wanachama wanaomiliki asilimia 51. Tatizo jingine kubwa ni wanachama was Simba, wengi wao wapo kwa ajili ya maslahi binafsi badala ya maslahi ya timu, ndio maana wapo tayari kuuza kura zao, kutohoji Mambo muhimu ya klabu mfano mashabiki walichangishwa pesa za uwanja, taarifa ya mwisho zilisema zilifika milipni 62 lakini hazieleweki mchango umefikia wapi, pesa zimeenda wapi.maana hata kwenye mahesabu ya klabu hazipo. Nini maana ya kukaribisha uwekezaji wakati hamna mipango ya maana Kama kujenga uwanja huu haya Mambo wanachama wanashindwa kuhoji.
Timu imeruhusu kuendesha na wanasiasa wakati wamiliki ambao ni wanachama wamekaa kimya.
 
Kipindi mnachukua makombe Bwana KIGWANGALA alikuwa anawaambia ukweli kuhusu Monasema awaachie MO wenu!! Nyie Mambo ya pesa sio mhimu kikubwa mhimu ni furaha ma makombe....!, Sasa furaha haipo makombe hayapo mmekengeuka😅.
 
Tatizo namba 1 la Simba ni Mo, yaani hapa mkuu umenena. Jamaa ni mpigaji asiyekuwa na huruma, bora hata GSM ana huruma ila sio Mo aiseee.

Namba 2, utawala wa nchi kwa sasa upo Yanga, ni ngumu sana Simba kutusua, hata msimu wa 2024/2025 bado Yanga atabeba tena makombe.

Akina Kassimu, Bashite n.k walikuwa wanaibebabeba sana Simba ktk tawala zao chini ya TFF.
 
Uyo Mo atakuja kuwaachia timu ambayo aina mwelekeo na ataiacha klabu ikiwa taabani maana aieleweki uwekezaji wake ni upi pale Simba na ni kitu Gani kipya amekiweka pale, awezi kusema ametengeneza uwanja sababu uwanja aliukuta ushanunuliwa na wakina Rage labda alichokifanya ni kulipia nyasi bandia zilizokuwa zimekwama bandarini walizokuwa wameagiza viongozi wa Simba, zaidi ya hapo akuna asset yoyote ya maana aliyoitengeneza yeye Kama mwekezaji!
 
ulikuwa sahihi[emoji123]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…