Simba is Business, Business is Simba

Simba is Business, Business is Simba

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Niwakumbushe tu kuwa Mamelodi Sundowns analipwa Rand Million 20 kwa Mwaka ni ni sawa na Rand Million 60 kwa mitatu kutoka Kampuni ya PUMA.

Mamelodi alipomaliza mkataba wake na NIKE hakuongeza tena na alitaka dili jipya lenye maslahi zaidi, hivyo PUMA anawapa sawa na BILLION MOJA kwa Mwaka.

Simba leo wamesaini mkataba na VUNJABEI nadhani ndio mkataba ghali zaidi kwa ukanda huu wa maziwa Makuu na hata kwa klabu za Afrika Kusini baadhi hazigusi mkataba huu mnono.

Simba atapokea BILLION MBILI, kwa miaka miwili ni sawa na MAMELODI ambaye pia anapokea BILLION kwa mwaka, nadhani tumeanza kuelewa thamani ya huu mkataba mkubwa.

Nadhani tumeanza kuelewa maana ya safari za Barbra kwenda Al Ahly na Mamelodi, hao ndio magwiji wa Afrika Kwenye mikataba ya hatari na mikubwa ya kibiashara barani Afrika, bila shaka kuna somo kalipata.

Mkataba huu ni hatarishi kwa SPORTPESA, Sote tunatambua kuwa SPORTPESA ndie Mdhamini Mkuu wa Simba, lakini kwasasa kazidiwa pesa Kwenye vitabu vya Simba kutoka kwa Vunjabei kwa hii BILLION MBILI

Maana yake ni nini? Thamani ya Simba imepanda maradufu, kama Sportpesa watataka kusalia kwa kandarasi mpya baada ya mwanzo kuisha ni lazima waanzie hapo kwenye Billion Mbili, hata Kampuni zingine lazima zianzie hapo kwenda mbele.

Wakati mpira unakuwa na Simba sasa inaenda mbele zaidi, hakuna kampuni itaenda kujadiliana na Simba kiwepesi sasa hivi, hiyo ni kanuni ya soko ELASTICITY OF THE BUSINESS, tayari Simba kuna hatua wamepiga.

Kwa Vunjabei tayari ana soko kubwa sana, anajua kuhusu Mavazi, mwisho hii ni WIN WIN SITUATION.
 
“Nitoe shukrani kwa uongozi wa Simba na kwa Wanasimba. Naamini wamerudisha tumaini jipya kwa vijana wengi. Tunaenda kutengeneza vitu vingi kama jezi, t shirt, cover la simu, miwani, saa za Simba, kofia, soksi, viatu, mabegi na vitu vingi.”- CEO wa Vunja Bei, Fred. #NguvuMoja

Nimependa hii ikiwezekana hadi condoms.
 
“Nitoe shukrani kwa uongozi wa Simba na kwa Wanasimba. Naamini wamerudisha tumaini jipya kwa vijana wengi. Tunaenda kutengeneza vitu vingi kama jezi, t shirt, cover la simu, miwani, saa za Simba, kofia, soksi, viatu, mabegi na vitu vingi.”- CEO wa Vunja Bei, Fred. #NguvuMoja
Nimependa hii ikiwezekana hadi condoms
Ha ha mkuu hapo kwenye vifanyio kwa kweli waangalie manake nacho ni kifaa cha mchezo japo ni wa kitandani na sirini.
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka.... mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu.
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka. Mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu.
Inakuuma eeeh
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu
Watanzania wengi bado tuna mentality za kikoloni,kuona makampuni ya kibeberu ndio pekee yenye ufanisi. Au kuona wazungu peke yao ndio wanaweza kufanya biashara.

Tuelewe zama zimebadilika,na biashara inataka soko,na kampuni inaitaji uzoefu wa soko!! Ukiangalia kwa umakini zaidi makampuni makubwa ya vifaa vya michezo ya mabeberu, mara nyingi yanatumia udhaifu wa timu na management zao kusaini, mikataba ambayo kimsingi ukichunguza inakuwa hainufaishi timu, zaidi inayonufaika ni hizo Brand za kibeberu sisi tunaishia kujisifu tu kuwa tunafanya biashara na Nike sijui Adidas lakini kiuhalisia ni zeros bussiness!

Mimi nawapongeza kwanza vunja bei,kwanza wanatakuwa na faida moja kubwa wanalijua soko la mavazi la Tanzania kuliko kampuni hizo za kibeberu. Pili watafaidika na wingi wa mashabiki wa Simbasc waliopo hapa nchini ambao ndio wamewalenga hasa na wanajua hali zao za kimaisha hivyo ni rahisi kwao kutengeneza products ambazo zitaendana na vipato vyao!

Tofauti na makampuni ya kibeberu ambayo mara nyingi uwa yanashindwa kutengeneza bidhaa zinazoendana na hali halisi ya soko husika.

Mwisho Simbasc inawashabiki wengi hapa nchini vunjabei Nina uhakika amefanya uhakika utafiti wa soko vizuri,itakuwa ni faida kwake kama atachanga karata zake vizuri.

Nawapongeza Simba SC kwa kuangalia fursa kutoka kwa vunjabei na kuitumia aina maana unakuwa unafanya biashara na kampuni yenye jina kubwa uku unapata fedha kidogo.
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu
Ila jamaa una WIVU sana wewe.
 
Hivi najiuliza mtu mzima na p*umbu zake anasema eti adida sijui puma sijui nike. hivi mnajua bei za jezi za kampuni hizo. Nendeni mlimani pale jezi 180,000 - 250,000 nani ana ubavu wa kununua hizo. Huoni utatengeneza nafasi ya watengeneza jezi feki kutamalaki.
Simba wameangalia mengi kulingana na kipato cha mtanzania wa kawaida.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Huyu chinga ameua asisahau na vitu vya nyumbani, condom, electronic viwe msimbazi tupu.
Ila utopolo watakuwa wamenuna sana walipo sikia habari hii
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka.... mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu.
Endelea na fikra zako za kimasikini kua kila kitu kizuri lazima kifanywe na mzungu.
 
Akiprint jezi laki 5 mara 30000 maana yake ataingiza bil 15
Ukitoa bilion 2 ya simba na labda gharama za matengenezo bilion 6

Anabaki na faida ya bilion 7 hiyo ni minimum
Mkuu ulisoma shule gani inayofundisha mambo rahisi namna hii?
Yaani wewe umechukulia kuwa hizo jezi VB anazipata bure kabisa.
Unashindwa hata kujua malighafi ya jezi atanunua. Pia kuna gharama za usafirishaji na usambazaji. Achilia mbali kodi kibwena za nchi hii. Pia kumbuka hiyo bei hawezi kuuza yeye ikiwa jezi zitasambazwa kwa mawakala mikoani na kuuzwa kwa wanaouza rejareja.
Halafu umesahau kuwa na mzigo haimaanishi utauzika wote, kuna kuharibika, kupotea, changamoto za kiuchumi kwa wateja, n.k
Pia uuzwaji wa jezi utategemea na utendaji wa timu (performance) kwa siku zijazo. Hapa VB wametake risk kwani ikiwa simba itakuwa na matokeo mabovu uwanjani itakuwa ngumu kwa jezi kuuzika.
Kwa kifupi hiyo bil 7 ya faida hakuna namna anaweza kuipata hata iweje.
Ni kweli atapata faida kubwa maana ndio malengo ya biashara yoyote lakini pia kumbuka hata asipouza bado Simba watapata bil 2 yao tu.
 
Kampuni kubwa ya vifaa vya michezo duniani Puma atoe bilioni moja kwa mwaka kwa timu kubwa ya mamelodi iliyopo nchi yenye purchasing power kubwa ya afrika kusini.

Mnaongeza sifuri kama wasanii wa bongo fleva, kisha mtudanganye muuza ronya ambaye hana hata audited financial statement nae anatoa bilioni moja kwa mwaka.... mnajua bilioni 1 ni sawa na milioni moja moja ziwe 1000, sasa huyo vunja bei anazitoa wapi hizo hela? Purchasing power ya watanzania unajua ikoje? Ndio maana hao kina puma, nike, adidas hatuwamudu.
Acha wajitekenye na kucheka wenyewe...
wapuuzi kweli
 
Bilion mbili ni hela ya kawaida, watu kila siku wanananunua magofu kariakoo kwa bei hiyo na zaidi na kuyavunja na hakuna anaeshangaa.
 
Akiprint jezi laki 5 mara 30000 maana yake ataingiza bil 15

Ukitoa bilion 2 ya simba na labda gharama za matengenezo bilion 6.

Anabaki na faida ya bilion 7 hiyo ni minimum
Na ndivyo biashara inapaswa iwe mkuu hasa ukiwekeza pesa ndefuu kama alivyofanya kijana mwenzetu fred
 
Back
Top Bottom