Simba isimuache Saido Ntibazonkiza bado ana mchango mkubwa sana

WANA SIMBA wote wana HASIRA na tulisha ambiwa tusiwe tunatoa maamuzi tukiwa na hasira au furaha...
 
Mwanzoni nilidhani tatizo la Simba ni mwekezaji, viongozi na wachezaji. Kumbe hata washabiki nao ni tatizo
 
Japo mimi siyo Simba lakini linapokuja suala la kweli nabaki na kweli. Saidoo ni mchezaji wa muhimu sana kwa wachezaji waliopo hapo ukoloni.
Endapo watamwacha watakuwa wameachia mali na watazikumbuka sauti zetu.
Umri siyo tatizo wampime kwa kile anacho deliver uwanjani na kwenye kapu lao mwisho wa msimu.
Nikitaka kuwa mkweli Saidoo amenikera sana kwa jinsi alivyocheza kwa kujituma hapo Simba kuliko alivyocheza timu yangu ya Yanga.
 
Isingeenda shirikisho maana yake nikwamba ata nafasi ya 3 isingepata.Kwasababu ilo shirikisho lenyewe simba imelipata ukiwepo mchango wa saido ambaye wewe unamwona hafai.Swala la ubinafsi ilo ni swala la walimu kwasababu wao ndio wanaowaona wachezaji kwa karibu kuliko sisi watazamaji.Ukitaja wachezaji 3 waliojituma uwanjani kwa simba hii iliyomaliza ya 3 jina la saido haliwezi kukosekana.Tumpe haki yake.
 
Wabongo sisi ni fuata upepo tu.hatuna muda wakufanya logic.Kuna watu wanamchukia ila wengi wao hawana sababu za msingi.Kama ambavyo kuna ambao walikua wanamchukia aziz k bila sababu hadi kumtukana uko mitandaoni.
 
Goal za penalty nazo ni za kujivunia kweli.
 
Furaha ya shabiki yyt ni kuona timu yake inanyanyua makwapa, vinginevyo kila shabiki anakuwa na hasira sana kwa namna yyt atayoona inamfaa kutema nyongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…