Simba itaimarika lini? Leo Kessy anatinga uzi wa Yanga



Kessy kama kaja yanga ni njaa zake hatujamuiba simba
 
Mkuu, asante kwa taarifa hizi. Inaonekana na fedha ndefu lakini bahati nzuri ulitoa mfano wa Katumbi au tusiende mbali Azam hapa Tanzania.
Hela anayotumia Katumbi au mzee Bakhresa kwenye usajili, mishahara, usafiri nk ni kiasi gani kwa mwaka mzima?

Hapo nimeacha makusudi ile initial investment kama uwanja nk. Chelsea kwa sasa wanaweza kuwa wanapata faida kwa maana ya matumizi na mapato ya mwaka. Imechukua miaka mingapi? Na usisahau wanaingiza fedha toka vyanzo vingi tu ukiacha hela za mlangoni. Hela ya Roman sidhani kama itarudi kirahisi.

Unayo idea budget ya kuendesha timu kama Simba kwa mwaka ni kiasi gani?
 
Kuna rafiki yangu mmoja ana WIVU sana....huwa anaongeaga hivyohivyo kama ulichokiandika wewe hapo.
 

Una uhakika Yanga hakuna mkakati wa kucheza hatua ya makundi? Basi wewe ni shabiki wa vijiweni. Simba inamhitaji sana mzee Kilomoni. Aliongea point za maana sana.

Pia suala la kumwaga pesa, unavijua vyanzo MUHIMU vya mapato ya klabu? Kwa huo mtazamo wako finyu unadhani Swansea inastahili kusajili wachezaji wa nje wakati haitarajiwi japo tu kushinda FA achia mbali klabu bungwa?

Ni muda sasa wapenzi wa Simba mkawawajibisha viongozi wenu kwa lengo la kujenga kikosi bora cha muda mrefu, badala ya kujikita kwenye propaganda. Soka ni ukweli
 
Mkuu, asante kwa taarifa hizi. Inaonekana na fedha ndefu ...
Unayo idea budget ya kuendesha timu kama Simba kwa mwaka ni kiasi gani?
Kuna source nimeipata hapa, ni sh. bilioni 3.008 (ya mwaka 2014/2015). Kumbuka hayo sio mahitaji, ni bajeti (maana yake walikuwa na uhakika wa kupata na kutumia hizo 3b bila kushiriki michuano ya kimataifa, so wangeshiriki na kutinga hizo hatua ingekuwa ni nyongeza, provided that umeondoa gharama za kushiriki)

 
...Swali zuri kabisa,km Yanga inaendeshwa kwa hela za Manji kwanini timu asipewe Dewji?!
Sababu viongozi wa Simba ni matapeli wapiga dili.

Kitu anasahau huyo ndugu yetu ni kwamba hata hela kiasi wanayopata Simba kama ambavyo wanapata Yanga, wajanja wanakula bila aibu. Ni kweli Manji anachangia hela zake pale Yanga lakini kwanza amehakikisha mapato halali ya club hayaingii mifukoni mwa wajanja.
 

Nazungumzia actual expenditure kwa mwaka. Kwenye budget kuna ngonjera na mbwembwe kuliko matumizi/mapato halisi.

Udhamini wa Yanga na Simba karibia ni ule ule tu. Mapato ya mlangoni hayapishani sana. Sasa tofauti iliyopo ni kwamba hela za Simba zinapigwa na wajanja wakati kwa upande wa Yanga, kwanza mapato yanasimamiwa vizuri kabla ya Manji kuweka hela yake. Tofauti iko hapo na ndiyo ilikuwa mpango wa Wambura.
 

wewe ni wa ajabu kweli,ulitaka wachezaji wapewe kadi na maua ili wajisajili
 
Ukizungumzia bajeti, maana yake unazungumzia mapato na matumizi, na yanatakiwa yabalance. So kama interest yako ni kujua expenditure, ndio hiyo iliyotolewa officially. Si rahisi kushawishi watu kuwa matumizi ya Yanga yanatokana na mapato ya klabu bila hela ya mtu mmoja

SOMA HAPA
 
Mkuu, soma tena nilichoandika hapo juu. Nimesema kile kiasi kinachopatikana, kinasimamiwa vizuri kabla Manji ajaweka hela yake. Ni dhahiri Manji anatoa hela kwa Yanga.
 
Wa Azam wanasajiliwa kwa kujitolea? Wanafika raundi ya ngapi?
 
Kiukwel kuna siku nilimfuatila Dewj akiwa anahojiwa kuhusu suala la simba, kama angepewa simba wangekuwa mbali sana simba
 
Simba walibugi sana kumfungia Kessy sasa wanalalama tena
 
Kila siku mnaongeaga hivi hivi mtaendelea kuwa wa Matopeni nyie wa Hapa Hapa fc.
Wameondoka wangapi na Simba ipo,Mchukueni akawasaidie kama mliweza kumnunua mnamuamini vipi kama hatowauza?
 
Mkuu kweli simba ipo hakuna anaebisha lkn simba kwa ubora wake ni sawa na mwadui ya Julio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…