Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Imekuwa wimbo na ngonjera zinazoimbwa na mashabiki wa Simba kila mara Yanga inapofanya vizuri dhidi yao au michuano ya ndani ya kwamba, Yanga haiwezi michuano ya kimataifa na wao wamewekeza uko.
Sasa ni dhahiri shahiri kichaka hicho kinaanza kufyekwa taratibu na kitafyekwa kabisa siku siyo nyingi kwa mipango madhubuti ambayo timu ya wananchi wanayo kwa sasa kuelekea hatua ya makundi ambayo itaanza mwezi wa 2.
Kwa mipango iliyopo ikiwemo kuboresha kikosi dirisha dogo kwa kunasa vifaa vya nguvu, nawaona Yanga wakiendelea kuwa bora kwenye hii michuano na sitoshangaa wakiivunja rekodi ya Simba ya kuishia robo fainali.
Siongei kwa kubahatisha bali naongea kwa kujiamini na mipango iliyopo kwa sasa, Yanga walikuwa wanahitaji sana wafuzu makundi ili wajipange vizuri kwa kuwa kuna kama miezi 3 kabla ya hatua ya makundi kuanza rasmi. Hivyo kuna mwanya wa kufanya usajiri dirisha dogo kuboresha maeneo muhimu.
Kwa maana hiyo naiona Yanga ikienda kutawala soka la ndani na nje ya nchi muda siyo mrefu, kwakuwa ni timu inayojengeka kwa kasi kubwa ikichagizwa na uwekezaji usiyokuwa na changa la macho wala ujanja ujanja.
Hii post itakuja kukumbukwa iheshimiwe.