Simba kufuru:Ngoma abugizwa 180m,kusaini mda wowote

Simba kufuru:Ngoma abugizwa 180m,kusaini mda wowote

Habari kubwa iliyonifikia hivi punde ni kwamba striker Donald Ngoma anatarajiwa kusaini mda wowote katika Club kubwa ya Simba.

Inasemekana Ngoma yupo katika mazungumzo ya mwisho na tajiri kijana Mohammed Dewji,na mda wowote atamwaga sahihi
Point za FIFA imekuaje
 
sijawah kuona klabu ina sajiri first eleven ktk dirisha la usajiri moja hapo kuja watengeneze combination league inaelekea mwisho mtawafukuza wote tena nxt season muanze upya, napata mashaka pia kumbe hata kukosa ubingwa mlijua mna team mbovu ingekua nzuri kuna haja gan ya kusajiri wachezaji wengi kias hicho
 
Nadhani wengi wanasahau kwamba usajili huu wa sasa kwa timu ya Simba ni muelekeo wa mashindano makubwa ya Kimataifa, maana kwa hali hii tayari VPL msimu ujao ni kwa Simba tu, noway
Hata mwaka jana mlisema hivi hivi
IMG_20170520_210528.jpg
 
Hiii ya Ngoma na yenyewe kama kweli vile. huyu jamaa akiwa katika ubora ni bonge la straika
 
Daah huyo Ngoma mbona ni wa kawaida sana aisee na pia injury zinakuwa hazimwendei mbali kama Sturridge wa liver nadhani simba watakuja kujuta sana baadae wasipokuwa makini kipindi hiki cha usajili maana si kwa matumizi hayo na pia wangejaribu kutazama performance ya mtu msimu uliopita kuliko kutazama jina hiii itawacost.
Zile sio injuries za kweli ni mgomo kwa sababu hajalipwa
 
Ndio zilikuwa swaga zao hizo huku wakidai Yanga tunasajili wazee! Nashangaa sasa hivi wanawasajili hao waliowaita madingi kwa mamilioni! Simba ni mambumbu daima!
Kama simba mbumbumbu wewe ni juha mpumbavu
 
SHIDA MOJA NABWEGE WA MSIMBAZI WANASHANGILIA USAJILI HAWA HAWA MWISHO WANATUKANA TIMU KUKOSA UBINGWA KHA AMKUJUA FEDHA AINUNUI KOMBE
 
Habari kubwa iliyonifikia hivi punde ni kwamba striker Donald Ngoma anatarajiwa kusaini mda wowote katika Club kubwa ya Simba.

Inasemekana Ngoma yupo katika mazungumzo ya mwisho na tajiri kijana Mohammed Dewji,na mda wowote atamwaga sahihi
img-20170627-wa0000-jpeg.531448

KickOff.com can confirm that Polokwane City
have completed the signing of Zimbabwean
striker Donald Ngoma.
The 27-year-old has penned a three-year deal
with Rise and Shine after undergoing a medical
with the Premiership side.
Ngoma is set to join the MTN8 participants as a
free agent once his contract with Young Africans
expires at the end of June.
Meanwhile, midfielder Tlou Segolela and veteran
hitman Esau Kanyenda are on the way out of
City, according to a source close to the club
"Ngoma's deal is done. It's a three-year
contract," says the source.
"He was here in the country for a medical
recently and now the paper work has been
done."
 
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amehitimisha miaka yake miwili ya kucheza Yanga ya Tanzania, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Polokwane City ya Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Polokwane, Ngoma mwenye umri wa miaka 27 sasa, amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Na Ngoma anajiunga na timu hiyo iliyofuzu michuano ya MTN8 kama mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake Yanga ya Tanzania mwezi huu.
Na baada ya kumpata Ngoma, Polo City inawatema kiungo Tlou Segolela na mkongwe Esau Kanyenda.


Ngoma alikuwa na msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.
Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu.
Na anakwenda Afrika Kusini, huku nchini Tanzania kukiwa kuna habari anakuja kesho kujiunga na mahasimu wa Yanga, Simba.
 
Naona Mikia wanajiimarisha kutetea kombe lao la FA maana VPL mwenyewe anajulikana.
 
Back
Top Bottom