Simba kuifunga Yanga siyo kipimo sahihi Cha kujiamini kuwa wao ni Bora dhidi ya wydad Casablanca

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Hakuna asiyejua kuwa mchezo wa derby wowote pale duniani hata ukiwa Bora namna gani unaweza ukafungwa tu.
Naikumbuka yanga akina balama mapinduzi na ditram nchimbi (yanga tia maji tia maji) yanga ya kupitisha bakuli lakini lilipofika kwenye suala la derby yanga ilitunisha msuli mbele ya simba ya akina miqson na medie kagere.

Hiyo ndiyo Derby unaweza ukawa Bora lakini ukapigwa kipigo kitakatifu bila ya kutegemea.
Simba imeifunga yanga kwa goli mbili sifuri,
Simba sc haipaswi kuchukua matokeo yao dhidi ya yanga na kwenda nayo kimataifa nakuona kwamba wanamuweza wydad Casablanca.

Simba ifute matokeo hayo kimataifa iende kwa heshima/kuwaheshimu wydad Casablanca Tena kwa nidhamu kubwa sana lakini ikiamua kuingia na matokeo mfukoni, kitakacho wakuta ni zaidi ya rajacasablanca alichokifanya kwa mkapa.

Ili niwe na Imani na Simba sc kuingia nusu kimataifa ni mpaka atakapo wafunga wydad Casablanca goli zisizopungua nne au nakuendelea tofauti na hapo Simba isipoutumia vizuri uwanja wa nyumbani (kwa mkapa) basi itakua imekosa tiketi ya kufuzu nusu fainali kimataifa.
 
Kwahio unashauri mashabiki wa mnyama tuwe wanyonge na tuseme tumeshatolewa na wydad ama tususie mechi? Twambie mkuu.
 
Mkuu sijui wewe Ni mpumbavu wa kiwango gani.

Hiyo Yanga iliyo bora Tena inacheza kombe la luza ilimfunga Nani goli 4

Kwahiyo unaona ubora wa Simba Ni kumfunga Wydad goli 4.Kwako Ni Jambo jepesi.

Kwanini wewe Ni mpumbavu?
Huyo Wydad na ubora wake tangu aanze mashindano ya mwaka huu kamfunga Nani goli 4.?

Huna Cha kuandika kuhusu litimu lako la Yanga?
 
Punguza makasiriko popoma wewe [emoji41] unakimbilia MATUSI bila kutafakari nilichokiandika.
 
Hapo umeona neno shabiki ?? Rudia kusoma tena
Nimerudia kusoma, unasema simba wasiende na matokeo mfukoni na wasijipe moyo kwamba watamfunga wydad kama walivyomfunga yanga, swali langu lipo palepale, kwahio hao simba unaowazungumzia unataka waanze kuambizana hatuwawezi hawa waarabu na tunakwenda kukamilisha tu ratiba? Tuambie mkuu.
 
Aliye kwambia kuwa Simba imerizika kisa kuifunga yanga ni nani?
Au mnadhani viongozi wa simba wana ulimbukeni kama viongozi wenu wa utopolo ambao baada ya Utopolo kuifunga Mazembe iliyo jifia basi wakaona wamemaliza kila kitu?
Simba huwa inaichukulia mechi ya dabi kama mechi zingine tu.
 
Tatizo unatumia makamasi kujibu hoja juu ya kile nilichokizungumza
 
Mnajifariji Sana utopolo. Simba kamfunga yanga' underdog akiwa ni yanga. Fuatilia makampuni ya kubashiri underdog alikuwa ni yanga'. Kwa hiyo Simba kushinda alistahili Kwa sababu ni Bora kuliko yanga.
Yanga kupewa odds nyingi siyo tafsri kuwa yanga ni underdog mzee tafuta hoja nyingine.
 
Yanga kupewa odds nyingi siyo tafsri kuwa yanga ni underdog mzee tafuta hoja nyingine.
Kupewa odds nyingi maana yake una chance ndogo ya kushinda.
Underdog maana yake mshindani mwenye chance ndogo ya kushinda. Bado hujaelewa?
 
[emoji2][emoji2] washajiona wako juu zaidi ya wydad..kitakachokuja kuwatokea Niko pale airport kuwapokea.
 
Sasa kwa akili yako ndogo ya kiutopolo unafikiri tunaweza kujipima kwa katimu kanachoshiriki kombe la waliofeli?????
 
Reactions: BRN
Pale bwamdogo anapomfundisha mkubwa jinsi ya kuruka dimbwi la maji, inachekesha sana kwakweli.
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…