Tuseme Ndanda wamekurupuka hawajui kanuni hata kidogoTunapoendekeza ushabiki pasipo kujua taratibu, hapa naona kila mmoja anavutia kwake! kuna wale wanaoomba Simba wanyang'anywe points ili wawe kileleni na kuna wale wanaoona wako sahihi kutetea ili kuendelea kuongoza ligi lakini kwa maoni yangu sioni ni kwa namna gani Simba itapokwa points!
Acheni ushabiki ktk kufanya maamuzi ya msingi@
Hili suala sidhani kama ni la michezo, ni suala la jinai ambalo wahusika ni Idara ya Uhamiaji, ni sawa na lile suala na Ndanda Kosovo na wenzake ambao walishitakiwa na kuswekwa gerezani kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali hadi wakatunga ule wimbo 'Jela ni mbaya' na kujiita Wajelajela.
Kwenye soka, muhimu no ITC tu, na ndio maana wamepewa leseni na TFF baada ya kuridhika kuwa wamehamishwa kihalali kutoka timu zao walizochezea msimu uliopita,TFF hawahitaji kibali cha kufanua kazi nchi ili watoe leseni, hilo ni suala la sheria za nchi. Ni mtazamo Wangi tu.
Vv
Jibu rahisi la swali lako ni Ulaya kanuni hiyo ipo husajili mchezaji mpaka awe na work permit. Hapa Bongo tunakurupuka tu. Hamna kanuni hiyo kwenye sheria zinazosimamia mpira nchini.Mbona huko ulaya wachezaji hawaruhusiwi kucheza bila work permit? Tena hiki huwa kikwazo kikubwa!!!!
Work permit ndio inafuata leseni. Huwezi kutoa leseni ya kuruhusu mchezaji acheze halafu ndio udai work permit wakati mchezaji umeshampa leseni.Hapo napata utata. Kipi kianze? Leseni ili apate permit au permit ili apate leseni?
NI kama vile kufaulu vipimo vya afya. Mchezaji anakuwa na kila kitu subject to the results of a medical checkupWork permit ndio inafuata leseni. Huwezi kutoa leseni ya kuruhusu mchezaji acheze halafu ndio udai work permit wakati mchezaji umeshampa leseni.
Fisi anangojea mkono udondoke. Mpira umewashinda. Wenzako wapo jangwani wanafanya mazoezi ya kupiga magoti ili wachezaji walipwe mishahara.
Wamesahau
Mmesahau suala la Kessy mlivyokuwa mna ng'ang'ania Yanga SC apokwe points za mechi ambazo Kessy kausika!!!!!
Au mmesahau?
[emoji23]
Klabu ndio inatafuta WP. TFF haina majukumu hayo.... [emoji23]tff wanatoaje lesseni bila work permit
Nadhani atakuwa ameelewa sasa!Hapo napata utata. Kipi kianze? Leseni ili apate permit au permit ili apate leseni?
Ningependa zaidi watani zetu Simba FC wasipokonywe point ili upinzani uzidi kuwa mkali.
-Japo ni kosa, lakini nawaombea watani walimalize hili bila kupunguziwa point, natafurahi watani tukimbizane point uwanjani kwa uwezo wa kisoccer.
Suala la Kessy kwa Yanga SC sio fitina....ikifanyika hivyo itakuwa ni mojawapo ya fitina