Simba kupokwa point za Ndanda?

Simba kupokwa point za Ndanda?

Tunapoendekeza ushabiki pasipo kujua taratibu, hapa naona kila mmoja anavutia kwake! kuna wale wanaoomba Simba wanyang'anywe points ili wawe kileleni na kuna wale wanaoona wako sahihi kutetea ili kuendelea kuongoza ligi lakini kwa maoni yangu sioni ni kwa namna gani Simba itapokwa points!

Acheni ushabiki ktk kufanya maamuzi ya msingi@
Tuseme Ndanda wamekurupuka hawajui kanuni hata kidogo
Kamati husika ije na majibu haraka kukata mzizi wa fitna
 
Hili suala sidhani kama ni la michezo, ni suala la jinai ambalo wahusika ni Idara ya Uhamiaji, ni sawa na lile suala na Ndanda Kosovo na wenzake ambao walishitakiwa na kuswekwa gerezani kwa kosa la kufanya kazi nchini bila kibali hadi wakatunga ule wimbo 'Jela ni mbaya' na kujiita Wajelajela.

Kwenye soka, muhimu no ITC tu, na ndio maana wamepewa leseni na TFF baada ya kuridhika kuwa wamehamishwa kihalali kutoka timu zao walizochezea msimu uliopita,TFF hawahitaji kibali cha kufanua kazi nchi ili watoe leseni, hilo ni suala la sheria za nchi. Ni mtazamo Wangi tu.

Vv

Mbona huko ulaya wachezaji hawaruhusiwi kucheza bila work permit? Tena hiki huwa kikwazo kikubwa!!!!
 
Ningependa zaidi watani zetu Simba FC wasipokonywe point ili upinzani uzidi kuwa mkali.
-Japo ni kosa, lakini nawaombea watani walimalize hili bila kupunguziwa point, natafurahi watani tukimbizane point uwanjani kwa uwezo wa kisoccer.
 
Mbona huko ulaya wachezaji hawaruhusiwi kucheza bila work permit? Tena hiki huwa kikwazo kikubwa!!!!
Jibu rahisi la swali lako ni Ulaya kanuni hiyo ipo husajili mchezaji mpaka awe na work permit. Hapa Bongo tunakurupuka tu. Hamna kanuni hiyo kwenye sheria zinazosimamia mpira nchini.
 
Hapo napata utata. Kipi kianze? Leseni ili apate permit au permit ili apate leseni?
Work permit ndio inafuata leseni. Huwezi kutoa leseni ya kuruhusu mchezaji acheze halafu ndio udai work permit wakati mchezaji umeshampa leseni.
 
Work permit ndio inafuata leseni. Huwezi kutoa leseni ya kuruhusu mchezaji acheze halafu ndio udai work permit wakati mchezaji umeshampa leseni.
NI kama vile kufaulu vipimo vya afya. Mchezaji anakuwa na kila kitu subject to the results of a medical checkup
 
Fisi anangojea mkono udondoke. Mpira umewashinda. Wenzako wapo jangwani wanafanya mazoezi ya kupiga magoti ili wachezaji walipwe mishahara.

Mmesahau suala la Kessy mlivyokuwa mna ng'ang'ania Yanga SC apokwe points za mechi ambazo Kessy kausika!!!!!

Au mmesahau?
[emoji23]
 
Mmesahau suala la Kessy mlivyokuwa mna ng'ang'ania Yanga SC apokwe points za mechi ambazo Kessy kausika!!!!!

Au mmesahau?
[emoji23]
Wamesahau
Huko kwa Kessy kulikuwa na kanuni lakini eti hili halina kanuni. Maadam kuna ITC na leseni basi mambo ya work permit haiwahusu.
We have a long way to go!
 
Tff wajaribu ujinga huo waone tunavyochukua pointi zte za yanga walizo mchezesha mchezaji wa simba hassan kesi
 
Ningependa zaidi watani zetu Simba FC wasipokonywe point ili upinzani uzidi kuwa mkali.
-Japo ni kosa, lakini nawaombea watani walimalize hili bila kupunguziwa point, natafurahi watani tukimbizane point uwanjani kwa uwezo wa kisoccer.

Watani huwa hawana moyo kama wato.... Wao hupenda miteremko mno..... Ndio maana wamekuwa wakipata shida sana kunyanyua makwapa.....

Kwenye Kesi ya Hassan Kessy walikuwa wanashinda kwa waganga wakiomba YANGA ipokwe alama... [emoji23]
 
ikifanyika hivyo itakuwa ni mojawapo ya fitina
Suala la Kessy kwa Yanga SC sio fitina....

Ila kwa upande wenu, mkiadhibiwa kwa kuenenda tofauti basi hiyo ni fitina..

Aisee
 
Back
Top Bottom