Muwe mnajifunza Sheria na Kanuni za Michezo ambazo zipo chini ya TFF na msitake kuyaleta ya Uingereza au huko Ulaya hapa Tanzania. Kanuni za TFF ili mchezaji wa Kigeni acheze mechi ya VPL ni mpaka awe na ITC tu na haisemi kuhusu Vibali vya kufanya Kazi hapa nchini kwani hiyo ni Kazi ya UHAMIAJI na siyo TFF na hata kama Klabu ya Simba itakutwa na hatia na UHAMIAJI ya kuwachezesha akina Daniel Agyei na James Kotei wote kutoka nchini Ghana bila kupatiwa working permit bado haitapokwa points zozote. Tuwe tunajikita sana katika kuzifuatilia Sheria na Kanuni za TFF ili siku nyingine tusije kuwa Watupu hivi kwa jambo jepesi tu kama hili.