Simba kupokwa point za Ndanda?

Simba kupokwa point za Ndanda?

Zulu alikuwa na ITC pamoja na leseni lakini viongozi waliona asicheze kwa kuwa work permit ilikuwa bado.
Bado najiuliza swali hilo hilo. Work permit ya nini Kama mchezaji akiwa na ITC/leseni anaweza kucheza?
Itakuwa kinyume cha sheria za nchi kucheza kwa maana kufanya kazi bila kibali husika.
Hizo ni kanuni duniani kote work permit ni muhimu kabla ya kufanya kazi nchi yoyote ile ya kigeni
 
Hizo ni kanuni duniani kote work permit ni muhimu kabla ya kufanya kazi nchi yoyote ile ya kigeni
Kuna watu wanajifariji eti maadam kuna ITC na leseni ya TFF basi
 
Ni kosa kubwa kwani hata kina pogba ilibidi wapate work permit ya uk ili waweze kucheza mu.
Jana nilimsikia msemaji wao akidai kuwa cha muhimu kwao ni kwamba wanayo ITC na leseni za wachezaji hao lakini alisahau kwamba ili wapate vibali vya kazi ni shuruti wachezaji hao wawe ni vitu hivyo 2.
 
Hizo pointi mtaishia kuzitamani tu! Chezeni mpira aisee! Hakuna kanuni ya kimpira iliyovunjwa, labda uhamiaji wawakamate wawatupe lupango kama wahamiaji haramu! Mpira wa Tanzania ni ridhaa, haujarasmishwa kuwa wa kulipwa kama hao mnaowafananisha!
 
Ni kosa kubwa kwani hata kina pogba ilibidi wapate work permit ya uk ili waweze kucheza mu.
Wewe wacha uongo. Unafikiri wote hapa wajinga kama wewe.Pogba ametoka Ufaransa ambao wapo EU,hahitaji work permit. Hili suala la work permit kwa wachezaji wanaocheza UK ni wale ambao Nchi zao hazipo kwenye EU na kwenye FIFA rankings wapo chini ya nafasi 75 au hajawakilisha Nchi yake kwenye timu ya Taifa.
Acha mambo ya matamko weka sheria ya TFF tuone hicho kifungu.
 
Hizo pointi mtaishia kuzitamani tu! Chezeni mpira aisee! Hakuna kanuni ya kimpira iliyovunjwa, labda uhamiaji wawakamate wawatupe lupango kama wahamiaji haramu! Mpira wa Tanzania ni ridhaa, haujarasmishwa kuwa wa kulipwa kama hao mnaowafananisha!
Kumbe work permit zina kazi gain?
TRA wanachukua kodi ukumbuke. Maana yake ni kazi. Ridhaa haina mshahara.
Tofautisha makaratasi na reality!
 
Na katika kuongezea una sign mkataba kutegemeana na kupatikana kwa work permit. Huwezi ukatoa leseni halafu ndio udai work permit.
 
Wewe wacha uongo. Unafikiri wote hapa wajinga kama wewe.Pogba ametoka Ufaransa ambao wapo EU,hahitaji work permit. Hili suala la work permit kwa wachezaji wanaocheza UK ni wale ambao Nchi zao hazipo kwenye EU na kwenye FIFA rankings wapo chini ya nafasi 75 au hajawakilisha Nchi yake kwenye timu ya Taifa.
The point ambayo amplify ni kwamba huwezi kucheza bila ya work permit unless kuna special treaty kati ya nchi involved.
 
Na katika kuongezea una sign mkataba kutegemeana na kupatikana kwa work permit. Huwezi ukatoa leseni halafu ndio udai work permit.
Unaweza kupata leseni na permit ikafuata.
Napenda kuamini kwamba leseni na ITC ni vitu vinavyohitajika kupata work permit na sio kinyume chake!
 
The point ambayo amplify ni kwamba huwezi kucheza bila ya work permit unless kuna special treaty kati ya nchi involved.
Hebu tutajie kanuni iliyovunjwa ya TFF. TFF wanatoaje leseni bila work permit ikiwa kanuni ni hiyo mnayodai?Ukishatoa leseni ni kwamba mchezaji anaruhusiwa kucheza. Sheria za kusimamia mpira zinaongozwa na kanuni sio matamko.
 
Kanuni na sheria za soka zinatungwa na kusimamiwa na TFF. Wao pia ndio waliopitisha kanuni inasema ili mchezaji wa kigeni acheze Tanzania anahitaji vitu viwili tu;

1. ITC
2. Leseni

Vyote hivi hutolewa na TFF kwa kushirikiana na mashirikisho mengine ya soka hasa kwenye ITC. Kwenye kanuni hakuna sharti la kibali cha kazi.

Tatizo lililopo hapa ni kuwa TFF haizingatii au kuwa sahihi zaidi haijaweka sharti la kutoa leseni lazima litanguliwe na kupata kibali cha kazi. Yaani huko mnakotolea mfano Ulaya na kwingineko mtu hapati leseni kabla ya kibali cha kazi. Huku kwetu TFF kanuni hiyo haipo. Wao wanataka ITC na kisha wanatoa leseni, mambo ya uhamiaji yameachwa kwa mamlaka nyingine. Huko tuendako, kanuni inabidi ibadilishwe ili kusiwe na mkanganyiko, lkn kwa sasa kwa mujibu wa kanuni HAKUNA ATAYEIPOKA SIMBA POINTI TATU.
 
Unaweza kupata leseni na permit ikafuata.
Napenda kuamini kwamba leseni na ITC ni vitu vinavyohitajika kupata work permit na sio kinyume chake!
Hizo kanuni unazodai zimeanza msimu huu?Kwenye kanuni zilizopo na zilizopita hakuna kipengele kinachosema kwamba mchezaji sio halali mpaka apate work permit. Nakupa homework ya kutafuta hiyo kanuni. Wachezaji hao kwa sheria za TFF hawajavunja kanuni yeyote.
 
Tunapoendekeza ushabiki pasipo kujua taratibu, hapa naona kila mmoja anavutia kwake! kuna wale wanaoomba Simba wanyang'anywe points ili wawe kileleni na kuna wale wanaoona wako sahihi kutetea ili kuendelea kuongoza ligi lakini kwa maoni yangu sioni ni kwa namna gani Simba itapokwa points!

Acheni ushabiki ktk kufanya maamuzi ya msingi@
 
Muwe mnajifunza Sheria na Kanuni za Michezo ambazo zipo chini ya TFF na msitake kuyaleta ya Uingereza au huko Ulaya hapa Tanzania. Kanuni za TFF ili mchezaji wa Kigeni acheze mechi ya VPL ni mpaka awe na ITC tu na haisemi kuhusu Vibali vya kufanya Kazi hapa nchini kwani hiyo ni Kazi ya UHAMIAJI na siyo TFF na hata kama Klabu ya Simba itakutwa na hatia na UHAMIAJI ya kuwachezesha akina Daniel Agyei na James Kotei wote kutoka nchini Ghana bila kupatiwa working permit bado haitapokwa points zozote. Tuwe tunajikita sana katika kuzifuatilia Sheria na Kanuni za TFF ili siku nyingine tusije kuwa Watupu hivi kwa jambo jepesi tu kama hili.
Yes, common sense is not so common! Ni hapo panaponisumbua.
TFF waseme mambo ya work permit haiwahusu ni kazi ya uhamiaji. It's non of their business.
Tusubiri matokeo ya pingamizi la wanakuchele .
 
Back
Top Bottom