Simba kutangaza utalii wa Tanzania kwenye CAF Chamipons League

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Huu ndio ujumbe uliopo huko Instagram, ambapo Mabingwa wa Nchi, Simba Sports Club kwa makubaliano maalum na Wizara ya Utalii, watavaa jezi zao zenye maandishi, "Visit Tanzania" lengo ni kutangaza kimataifa na kuwavutia wageni mbalimbali kuja kufanya utalii nchini.

Ikumbukwe wadhamini wa Simba, kampuni ya kamari itabaki palepale kama wadhamini wakuu wa klabu. Ila Simba hawatowatumia kwenye mechi za Klabu bingwa Afrika kutokana na sheria za kamari kubanwa na CAF.

Unaonaje mpango huu wa Simba? Big Yes or Big No?

 
Hii itaonekana tumeiga slogan ya Rwanda mkuu.

Yah ni kweli, lakini kuiga jambo zuri sio vibaya! Wenzetu Rwanda wamefanikiwa sana kwenye hilo, walianza kuidhamini Arsenal baada ya mafanikio sasa wameiongeza na PSG.

Ila tofauti ni kwamba Rwanda wanamwaga pesa kwenye zile klabu huku kwetu serikali ya mitano tena hawatoi pesa!
 
Hatua nzuri sana kwa wizara na Simba SC.

Kwa mdau aliyeeleza itaonekana kuiga kutoka Visit Rwanda sio kweli! Tanzania imewahi kuendesha matangazo ya namna hii Premier League kupitia Sunderland na Newcastle.

Vibao vya matangazo vilisomeka | Visit Tanzania, Visit Kilimanjaro, Visit Serengeti na See Zanzibar.
 
Wazee wa kucopy na kupaste
Hawa Manyani hayajambo kwenye copy and past, Mabingwa wanafanya media tour, wao wakaja na media day , cha ajabu sasa badala ya Wachezaji waende kujifunza jinsi media zinavyofanya kazi, wao wanawaita waandishi wawapige Picha Wachezaji wao wanapofanya mazoezi na kuogelea.

Niliwacheka sana waandishi waliokua wanasifia jinsi Utopolo media day ilivyoendeshwa. Ukweli ni kwamba kitendo kile kilikua kwa ajili ya kuwadharau waandishi wa habari kisa ubwabwa walioandaa.
 
Hapana bhn sisi ndiyo tulianza kabla ya Rwanda.
 
Kuwa ni bure sawa, ingekuwa kwa kulipia ingekuwa ni hasara kwa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…