Simba kuweni serious Matola hana uwezo wa kutufikisha mbali kimataifa

Simba kuweni serious Matola hana uwezo wa kutufikisha mbali kimataifa

Mleta made sio mtu wa mpira kadandia tu. Angekuwa mtu wa mpira asingedhani Selemani anaweza kuwa kocha mkuu Simba
 
Wachezaji wenye nidhamu mbovu waanze katwa mishahara...
 
Mleta made sio mtu wa mpira kadandia tu. Angekuwa mtu wa mpira asingedhani Selemani anaweza kuwa kocha mkuu Simba
Kweli mkuu! Yaani awe kocha msaidizi kule Lipuli na Polisi afu aende Simba kuwa kocha Mkuu! Haiwezekani kwa kweli, ingawa siipendi hii timu ya Bunju!
 
Nimeona tetesi za kocha Suleiman matola kuwa ndio anakuja kuwa mrithi wa Aussems,kiuhalisia kwangu sioni kama ni mtu sahihi kabisa,

Mimi sio hater wa matola bali ni mshabiki wake namba moja lakini katika suala la kuwa kocha mkuu Simba kwangu siafiki kabisa.Nina shaka na uwezo wake hasa kimataifa viongozi tafuteni kocha mwenye CV kubwa kimataifa,swala sio kuwa na wazawa ambao bado hawana viwango, Matola anafaa zaidi kuwa msaidizi ila sio kupewa ukocha mkuu hasa kwa Simba.
Kapewa nafasi ya kocha msaidizi. Ajabu atakuja kocha mkuu na kutaka awe na msaidizi wa chaguo lake. Mbilinge zitaanzia hapo.
We never learn.
 
Tetesi zilizopo kocha wa mamelod ndio chaguo namba 1 huko kagoma kuongeza mkataba hivyo Mr Senzo anaongea naye
Simba haina uwezo wa kumleta kocha wa Mamelod, ikiwa uyo Uchebe wa kulipwa dola 7000/= wameona nyingi wamemtafutia sababu za kumtimua.
 
matola ni mtaalam wa fitna na mipango mipango mingine kama kupanga panga matokeo nje wa uwanjaa, hivyo simba hongereni sana kwani sasa mmeamua kucheza fitna badala ya football!, nawahurumia sana
 
Simba haina uwezo wa kumleta kocha wa Mamelod, ikiwa uyo Uchebe wa kulipwa dola 7000/= wameona nyingi wamemtafutia sababu za kumtimua.

nimeshangaa na mimi.. mosimane huyu huyu kipenz cha wa south aje aajiriwe na Simba ya Tanzania
 
Tuache utani lakini, matola ni kocha mzuri t, mimk nasema wakiungana na Maxine itakuwa bonge la combination, tumeona mara nyingi anapo kutana na hao makocha wakigeni wanapota pata wakati mgumu, sana kumfunga pamoja na kubebwa na wachezaji wakigeni na wenye gharama kubwa.

It is time tuwaamini wazawa naamini matola na mexime waomeonyesha kuwa na uwezo mkubwa tu.
 
Tetesi zilizopo kocha wa mamelod ndio chaguo namba 1 huko kagoma kuongeza mkataba hivyo Mr Senzo anaongea naye
Wale jamaa walikuwa wanamlipa dola 56000 kwa mwezi,Na alikuwa namba 5 kwa hela nyingi Africa sasa nyie madogo mtaweza huo mpunga na tunaambiwa mnawajumbe wa bodi mbumbumbu sana
 
Kuna mwaka waliwahi kumchukua kocha aliewahi kuwa wa timu ya Taifa S.africa alikuja akakaa miezi haizidi mi3 akatimua aliwaambia timu ni unprofessional. Anaitwa Trott Moloto.
nimeshangaa na mimi.. mosimane huyu huyu kipenz cha wa south aje aajiriwe na Simba ya Tanzania
 
Back
Top Bottom