tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye hoja moja kwa moja lakini awali ya yote naomba ku declare intest kwamba mimi ni mwanaSimba kindakindaki. Nina imani Simba Day ya leo tarehe 19/9/2021 imeandaliwa vizuri kimkakati na kimipango lakini kuna jambo moja ambalo klabu imetukusea sisi mashabiki wa ukweli wa Simba. Tangu nilipopata taarifa kuwa mgeni rasmi wa siku ya leo ni mzee wa Galilaya, mnazaleti Job Ndugai, nimeamua nisiende kiwanjani. Naomba mashabiki wengine wa Simba mniunge mkono kususia tukio lhili la Simba siku hii ya leo. Hivi viongozi wa Simba huwa mnawaza nini hasa? Au Ndugai amewahonga hela ili awe mgeni rasmi leo kwa manufaa yake binafsi? Mnakwama wapi lakini?
Image ya Ndugai katika taifa hili imeporomoka sana kiasi kuwa hafai hata kuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya birthday. Iweje leo Simba mnamleta mtu huyu kuwa mgeni rasmi? Kusema kweli kitendo hiki kimeniuma sana na sio mimi tu, hata mashabiki wengi wa Simba watakuwa wamesikitishwa mno na kitendo hiki. Ombwe la Manara limeanza kuonekana mapema. Manara angekuwepo Simba hadi leo asingekubali kamwe ujinga huu kufanyika. Nasikitika kusema kwamba sitakwenda kiwanjani na wala sitafuatilia tukio hili kwenye TV. Nina kazi nyingi za kufanya siku hii ya leo. Kama nitakosa cha kufanya bora nilale usingizi.
Mlioumizwa na kitendo hiki cha Simba kumteua mgeni rasmi wa ovyo namna hii, tujuane mapema.
Nawasilisha.