Simba kwenda na Wachezaji 31 kimataifa huku Yanga wakienda na 28

Simba kwenda na Wachezaji 31 kimataifa huku Yanga wakienda na 28

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Simba imepeleka majina ya wachezaji 31 CAF. Makipa wanne ambao ni chaguo lao la kwanza Aishi Manula, Benno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim katika orodha hiyo.

Safu ya ulinzi ina mabeki tisa ambao ni; Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Kapombe, huku eneo la kiungo likiwa na watu 12 ambao ni Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Pape Ousmane Sakho.

Wengine ni Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute na Thadeo Lwanga, huku kwenye ushambuliaji kuna nahodha John Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu na Kibu Denis.

Yanga waenda na Wachezaji 28
Yanga inajipanga na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali wakikutana na Rivers United ya Nigeria na uhakika pale makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) upande wa Idara ya Mashindano yamefika majina 28 tu.

Orodha ya uhakika ambayo Mwanaspoti imeipata ni kwamba jina la mwisho kukamilishwa katika usajili huo ni kiungo Khalid Aucho ambaye Waarabu wa Lel Makkasa inayoshiriki Ligi Kuu Misri walikuwa wanadengua kutoa uhamisho wake wa kimataifa lakini baadaye wakaachia wenyewe.

Orodha ambayo Yanga imewasilisha inawajumuisha makipa 3 ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa 9 ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.

Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’ watakaosimamia uimara wa Yanga katika safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Yanga imewajumuisha viungo 6 ambao Mukoko Tonombe, Aucho, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko, Farid Mussa, huku kwenye eneo la ushambuliaji itakuwa na watu 5 ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.

Crediti: Mwananchi.
 
mbona simuoni Ditram Nchimbi au sio uto tena
 
Wakuu hivi Ibrahim Ajibu amekua converted kuwa mshambuliaji ?
Naona kwenye orodha mbalimbali za vikosi vya Simba anajumuishwa kama mshambuliaji.
Mimi nilikua nafahamu kwamba Cadabra ni kiungo mshambuliaji tena nambari kumi.

Naomba kutolewa tongotongo katika hili.
 
Back
Top Bottom