Yanga leo imecheza kikubwa na kuonesha wazi ni timu kali kuwahi kutokea duniani, Azam ulimi nje. Kwasasa tuko tayari kucheza derby makolo waje sasa tuwakande khamsa tu maana hakuna namna, wapigwe tu! Kwa boli tulilopiga leo chamazi, basi naomba viongozi wa Yanga mlegeze kamba tudai fidia tu kisha tukubalia kucheza na makolo maana ubingwa tayari ila ubingwa utanoga zaidi tukiwakanda Simba ili tuwakate kamdomo ka ushindi wa kuingia nusu fainali kombe la single mothers!
Ambacho sikupenda leo ni baada ya kuwatandika Azam bakora mbili safi bila majibu eti tukaanza kuwaonea huruma na kucheza kama mazoezi tu tukaacha kuwakabia juu na kuwakata pumzi, wale Azam walipaswa kula goli khamsa japo mwanangu ni Azam alichukia sana leo huku kavaa jezi nilizomnunulia! Kwa kupunguza nguvu ya kucheza baada ya kufunga goli mbili, si kila siku tutakuwa na bahati ya kusalia na ushindi Hadi kipyenga cha mwisho
Kocha Hamdi please aongeze mazoezi ya pumzi na kukimbia maana dkk 20 za mwisho Azam walisumbua sana na kupata bao. Ile intensity ya Ramovic irudi tena Yanga icheze kwa nguvu ile ile kwa dkk 90. Ikibidi kipindi cha pili nguvu iwe mara tatu zaidi kama kipindi cha kocha Nabi.
Azam waambiwe wapunguze rafu za kijinga kwenye mechi za Yanga, waache kukamia wachezaji wa uto, wataua vipaji, inaonekana ndio mbinu wamebaki nayo maana mpira umewashinda, Yanga ni Mlima mrefu kwao, rafu ya Mwaikenda kwa Prof Pacome imetuudhi sana wana utopolo wa Buza mpalanger na rafu ya Akaminko kwa Maxi Nzengeli ilikuwa mbaya mno rafu zote mbili zilistahili red cards, hawa tff hawana faida kabisa , tff wawakanye Azam waache rafu mechi za Yanga , mpira si vita ni burudani, Azam wacheze boli sio Kung Fu. Huyu Akaminko ashawahi kumuumiza Skudu na kumharibia kiwango. Huyu hafai kucheza NBC league.
Yanga bingwa!!
Wapi fataki za sheikh Amri Abeid!!