Simba mmesikia alichokisema Ajibu?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
STRAIKA mpya wa Yanga na kipenzi cha walio mashabiki wa Simba SC, Ibrahim Ajibu, tangu asajiliwe kutoka Simba hakuwahi kuzungumza lolote, lakini juzi Jumanne jamaa aliamua kufunguka na kutamka kauli ambayo Simba wakiisikia lazima wanune.

Ajibu amesema tangu atue ndani ya kikosi chake kipya, amekuwa mtu mwenye amani, akifurahia maisha na amewaahidi mashabiki wa Yanga mambo mazuri.

Straika huyo aliyeifungia Simba mabao 26 katika Ligi Kuu Bara kwa misimu mitatu aliyoichezea akiwa tegemeo, alisema anajisikia faraja kubwa kuwa Yanga na kwamba kuna mazuri yanakuja.

Ajibu anacheza nafasi ya ushambuliaji lakini sifa yake kubwa ni unyumbulikaji yaani ana uwezo wa kuuchezea mpira anavyotaka, pia ana uwezo wa kutembea uwanjani anavyotaka jambo ambalo ndiyo linalowafanya makocha wengi kumtumia kama straika namba mbili.

Mchezaji huyo kipenzi cha mashabiki, amesema: “Nahisi tofauti, tangu nimejiunga na Yanga nimekuwa mtu mwenye amani na ninafuraha, nashukuru tunaishi vizuri na wachezaji wenzangu na wananipa ushirikiano wa kutosha.

“Kwa ujumla nina furaha na imani yangu kazi nitakayofanya itakuwa nzuri, ninachowaahidi mashabiki ni mambo mazuri kuhakikisha Yanga inafanikiwa, huwa sipendi kuzungumza maneno mengi, wasubiri nitakachokifanya uwanjani, kikubwa nahitaji ushirikiano.”

Ajibu ndani ya kikosi cha Yanga amekabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Matheo Anthony na anatarajia kuanza kung’aa pale msimu mpya wa Ligi Kuu Bara utakapoanza mwezi ujao.
 
Kwanza Simba walimuokota mtaani wakamfundisha mpira Hana Hata shukrani huyu chokoraa
Hata kama mnamlipa pesa ya madafu? Msijisahau kuwa hawa nao wanafamilia zao....Pesa ni kipaumbele soka la bongo, otherwise utakufa masikini.
 
Ulitaka aiponde yanga au simba acha utoto hio kauli ya kawaida kwa mvhezaji maana yeye hana timu kila timu anaenda tu.
 
Ajibu ndio mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha mpira kuliko wote Tanzania...
 
lazma aipende kazi yake.. kuondoka simba sio tatizo nachomtakia mafanikio mema tu
 
Ajibu ndio mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha mpira kuliko wote Tanzania...
Then hayupo timu ya taifa ama ya AFCON au ChAN!!!


Nonsense

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Aache kiherehere, kwani ameshakaa miaka mingap sasa hapo YANGA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwacheni atapoa kama kaseke na kessi walivyopoa. Vyura hawawezi tunza kipaji chako. Ukipoa tu wanakupotezea. Acheni afurahi ila number ikipata mwenyewe atilia kuwekwa bench.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…