Simba msijisahau na kuendelea kusherehekea kuingia nusu,mkasahau kujiandaa na yajayo

Simba msijisahau na kuendelea kusherehekea kuingia nusu,mkasahau kujiandaa na yajayo

Lee Van free

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2024
Posts
2,833
Reaction score
8,777
Historia inatuonesha Kuna watu walisherehekea mafanikio wakasahau kujiandaa kwa matukio yajayo,mwisho wa siku wakaja kupoteza kirahisi kabisa.

Kitu ninachoweza kuwaambia, kwa kadri mtu anavyosonga mbele katika jambo lolote lenye faida, ndivyo anavyokutana na ugumu.

Hivyo nawashauri Viongozi wa Simba, mrudi kwenye maandaliza makali zaidi kuliko hata haya mliyofanya safari hii ili kuvuka robo fainali.

Ongezeni nguvu kwenye mikakati na maandalizi.

Kumbukeni Kila timu inapoingia hatua za juu kama hii, shauku na umakoni huongezeka, kwa Hali hiyo hata Stollenbosch nao wataongeza shauku na umakoni ili kutushinda sisi.

Bahati pekee tuliyonayo ni kwamba safari hii hatukutani na timu za Misri,timu ya Misri hata kama ikiwa dhaifu lakini wanapofika hatua hii hutumia Kila njia Kila hila kufuzu.

Ikumbukwe pia kua,Zamalek Wana hasira na Simba, kwa sababu Simba ilishawavua ubingwa na kuwatoa mashindanoni.

Hivyo mechi hiyo ingekua ni mechi ya kisasi.

Bahati nyingjne kwa Simba ni kua, Kocha Fadlu Davids ni raia wa SA hivyo anayajua vizuri mazingira na Tabia za timu za SA,ukiondoa kua ni raia wa huko Bali pia ni kocha aliesomea huko, na pia aliwahi kuwa mchezaji mpira wa timu ya ligi ya SA.

Haya ni mashindano ya vilabu na wala sio mashindano ya timu za taifa mpaka tuhofie kwamba pengine ataingiwa na uzalendo na kutamani kulisaidia taifa lake kwa kuhujumu taifa letu.

Fadlu anatafuta CV,anatafuta kujulikana,anatafuta fedha na anatafuta maisha Bora zaidi kimataifa.
Fadlu ana watu,nduguna jamaa alikua nao na alioishi nao huko, baadhi watatamani afanikiwe,
Ikumbukwe kwamba, timu nyingi hazipendani, kama vile Simba na Yanga zisivyopenda.
Simba bado ana safari ndefu yenye milima mkubwa.

Napenda nitoe onyo kua Stollenbosch ni timu Kali,nzuri na imara.

Lakini pia kuanzia Leo Simba tukumbukeni tulichofanyiwa na timu ya Stella Abidjan ya Ivory coast, katika fainali ya kombe la CAF, katika mechi ya marudiano,baada ya kutoka bilabila huko Abidjan, lakini tulivyorudi Dar, tukaja kupigwa goli Mbili bila na mchezaji Boli Zozo mbeli ya Rais Alhaj Ali Hasan Mwinyi mwaka 1993.

Hapa naomba umakini mkubwa Kwa sababu katika mashindano ya Kimataifa kati ya Simba na timu za nje,Simba hua tunacheza na timu mbili.

Timu ya nje na timu ya ndani Kwa pamoja.

Timu ya nje hua ni visible na timu ya ndani hua ni invisible.

Ukweli ni kwamba ,Simba bado inajenga timu.

Simba Ina wachezaji wengi wapya na kocha mpya.

Ubaya Ubwela.
 
Umeandika hoja lakini uandishi wako sio mzuri sana.

Pia ungeweza ku Summarise andiko lako ili iwe rahisi kueleweka hoJa ziko wapi.

Rekebisha uandishi
 
Wanaoshangilia ni mashabiki sio wachezaji
Mpuuzi wewe
Mimi ni Simba ndugu,ila nimependa kukumbusha TU,kama mshabiki ninayo Hali ya kutoa maoni yangu hata yawe ya kipuuzi namna Gani.
 
Umeandika hoja lakini uandishi wako sio mzuri sana.

Pia ungeweza ku Summarise andiko lako ili iwe rahisi kueleweka hoJa ziko wapi.

Rekebisha uandishi
Makolokolo Kungwi Mwandamizi si tulikubaliana yeyote anayeshabikia Simba na Yanga ni Mpumbavu kiwango cha SGR, mbona kila uzi wa hizo timu wewe ndiwe ki-front front kuchanganua hoja?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Simba anaenda kufungwa tena
 
Sasa Simba anakutana na Zamalek au Stollenboch ya South Africa. Zamalek ameshatolewa na kurudi zake Misri huko.
Kwa hio mleta mada ana changanya mada? Simba anakutana na Stollenbosch?
 
Kwa hio mleta mada ana changanya mada? Simba anakutana na Stollenbosch?
Kwanza umeonesha kabisa wewe mpira haufuatilii, pili hujasoma bandiko la mleta mada zaidi ya kukoment tu! Jenga tabia ya kusoma kitu kwanza na kukidadavua then utoe maoni yako. Haya some mtoa mada hapo nimemquote
"Kumbukeni Kila timu inapoingia hatua za juu kama hii, shauku na umakoni huongezeka, kwa Hali hiyo hata Stollenbosch nao wataongeza shauku na umakoni ili kutushinda sisi.

Bahati pekee tuliyonayo ni kwamba safari hii hatukutani na timu za Misri,timu ya Misri hata kama ikiwa dhaifu lakini wanapofika hatua hii hutumia Kila njia Kila hila kufuzu.

Ikumbukwe pia kua,Zamalek Wana hasira na Simba, kwa sababu Simba ilishawavua ubingwa na kuwatoa mashindanoni."
Umelewa sasa?
 
Hapo mimi nimeona Zamalek
 
Hapo mimi nimeona Zamalek
Ok kama umeona Zamalek na unafuatilia haya mashindano meaning ungeshafahamu kuwa Zamalek is no longer in the tournament baada ya kutolewa na hiyo team ya South Africa na kingine you could have some guts za kumrekebisha mleta mada. Alimtaja Zamalek kama sehemu ya kutumia chuki yake juu ya Simba kumpa siri za kimbinu Stollenboch kwasababu anaifahamu vizuri Simba maana ameshakuta nae mara kadhaa kwenye mashindano makubwa. Nadhani sasa tuko pamoja na mleta mada si ndivyo?
 
Tuko pamoja kabisa Simba anakufa tena 3
 
Back
Top Bottom