kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Hakuna kocha mzuri asiyekuwa na timu ya kuifundisha, na hakuna timu bora inaweza kuachana na kocha na mchezaji bora katikati ya msimu labda kwa dau kubwa la kufa mtu. Simba haina fedha ya kubwa ya kuzinyanganya timu bara wachezaji na makocha wao bora kabla ya mwisho wa msimu. Hamna haja ya kutafuta mwalimu mpya sasa badala yake watumieni Cadena, Matola, Mgunda na Julio kwa pamoja hadi mwisho wa msimu, mtaona maajabu ambayo hamkuyatarajia. Bila Simba tamu hakuna Yanga tamu.