Simba muwape wanachama wenu elimu ya mpira ili kuepusha maafa na presha kwa viongozi, muwaambie ukweli!

Simba muwape wanachama wenu elimu ya mpira ili kuepusha maafa na presha kwa viongozi, muwaambie ukweli!

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Ni jambo la hatari sana ambalo viongozi wa Simba wamekuwa wakilifanya bila wao kulitambua nalo ni propaganda badala ya ukweli na uhalisia wa mpira wa miguu.

Kwa Sasa hivi wanajinasibu kwamba wanatengeneza Simba mpya lakini hapo hapo wanashindwa kuwaambia ukweli wanachama wao ambao wanayo matarajio makubwa sana na simba kwenye kipindi hiki Cha usajili.

Siku zote unapojenga timu upya usitegemee mafanikio ya haraka lazima uwe mvumilivu kwa angalau misimu 3 mpaka 4 ili urudi kwenye ubora wako wa kupigania Mataji, mpira sio Kama ugali kwamba maji yanachemka unasonga hapo hapo unaiva na kula.

Kwenye ujenzi wa kikosi kipya lazima utakuwa na maingizo mengi ivyo Kuna wachezaji wengine wataclick na wengine wataferi kwenye wale uliowasajili Ivyo inakubidi usubili Tena dirisha jingine uwaondoe usajili Tena, hapo muda unaenda.

Pia Kuna suala la muunganiko wa wachezaji kucheza kitimu linachukuaga muda mrefu kukaa sawa ikiwemo kuielewa falsafa ya kocha husika nalo ni tatizo JINGINE.

Kuna suala la kuizoea ligi ya Tanzania kwa baadhi ya wachezaji pamoja na mazingira kwa wachezaji wa kigeni nalo pia ni tatizo.

Ivyo ukijumuisha ayo mambo kadha wa kadha unaona kabisa Simba ni lazima watapitia maumivu makali mpaka waje wakae sawa ivyo ni muhimu wawaandae wanachama wao na mashabiki kisaikolojia wasiwadanganye kwamba msimu huu wanapigania ubingwa ni uongo.

Yanga aliangaika karibu misimu 4 baada ya kuanza project mpya baada ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye timu, mpaka wamekuja kujipata imewachukua muda mrefu.

Tuko kuwa tunashuhudia maingizo ya wakina yikpe, molinga, sibomana, na wengine wengi ambao walikuwa ni magarasa lakini ilikuwa ni Mchakato wa kuelekea kwenye ubora.

Kwa maana iyo Ahmed Aly aache kuwaaminisha mashabiki wao vitu ambavyo kiuhalisia ni ngumu kufanikiwa kwa msimu mmoja ama miwili aache kuwa comedy badala ya kuwa msemaji, watakuja kumgeukia na Kuona na yeye ni mamluki Kama wanavyomsema mangungu.

Nawatakieni Kila heri bila kusahau kuwaambia kuwa ligi ya msimu ujao utakuwa ya moto Azam anaitaka nafasi ya pili kushikilia kwa mara nyingine Tena kwa namna wanavyojiimarisha kazi kwenu.
 
Yanga Walikuwa wanajitafuta ili Wajipate na ndio maana ilibididi Miaka zaidi ya Mi4 ipite kipindi Cha kina yikpe,Molinga nk.

Hata Kwenye Rank Walikuwa Wa 574...!

Sasa Simba Mpaka Sasa ni ya 6 Kwa Ubora. Haijitafuti ili ijipate... Simba ipo Kwenye Kuongeza tu Makali izidi Kwenda Juu kuelekea Tano Bora , nne na Hatimaye Kinara Wa Soka Afrika.

Bahati mbaya Wachambuzi wetu Uchwara wanaaminisha Simba inajitafuta... ! Sita Bora akijitafuta , 50 Bora Azam atakuwa anacheza Komborera Basi!!😁😁
 
Mitano ✊ mingine kwa Mwenyekiti Mangungu!!
 
Na hii ndio shida yenu kubwa wanazi wa Simba. Mmefunikwa sana na mahaba mnaukwepa ukweli, mkiambiwa kitu hamjipi nafasi kutafakari ni moja kwa moja kubisha!! Sikilizeni mkiambiwa kitu kisha ndio mu argue

Hivi unakumbuka mwaka jana msimu ulivyokuwa unaanza jinsi mlivyokuwa na confidence asee. Kila mwana Kolo alikuwa so happy na usajili na very confident baada ya kuaminishwa kuwa usajili ni bora kabisa
 
Kwasasa nimepunguza mapenzi na simba litakalotokea nikotayari. Yani maisha yaniumize kichwa na simba iniumize kichwa siwezi.

Wabakie wanaonufaika na simba ndio waumie sio mimi niliopo nanjilinji ndanindani huku.
 
Yani ahmed ally ameshaona wanasimba wote wajinga yani wanawapa matarajio makubwa mashabiki ila kinatokea nitofauti sasa utasikia leo saa nane tunajambo letu.

Da kinachopostiwa sasa ni ujinga mtupu. Viongozi kuweni wakweli hata hakuna hela ya usajili.mfano jobe na fred mmeshindwa kuwavunjia mikataba na huku mkijua viwango vyao ni vyakuungaunga.

Sasa kwataarifa yenu viongozi ,mwaka huu simba day itadoda labda muweke kiingilio buku tatu. Hata kama msemaji azunguke dar yote na kispika haitosaidia kitu.

Mashabiki wameshachoka uongo wenu naamini usajili wa mwaka huu pia utabuma.

..
 
Yanga Walikuwa wanajitafuta ili Wajipate na ndio maana ilibididi Miaka zaidi ya Mi4 ipite kipindi Cha kina yikpe,Molinga nk.

Hata Kwenye Rank Walikuwa Wa 574...!

Sasa Simba Mpaka Sasa ni ya 6 Kwa Ubora. Haijitafuti ili ijipate... Simba ipo Kwenye Kuongeza tu Makali izidi Kwenda Juu kuelekea Tano Bora , nne na Hatimaye Kinara Wa Soka Afrika.

Bahati mbaya Wachambuzi wetu Uchwara wanaaminisha Simba inajitafuta... ! Sita Bora akijitafuta , 50 Bora Azam atakuwa anacheza Komborera Basi!!😁😁
Wanachama wa aina hii ndio tatizo pale Simba na mangungu akuwa mjinga kuwaongoza ni rahisi sana
 
Mimi sina matumaini as long as kile kizee kipo.
Kusema kweli ninawasi wasi tu kinatumika kuihunumu timu ili kimfurahishe aliyekipigania kiwe kiongozi.
 
Kwasasa nimepunguza mapenzi na simba litakalotokea nikotayari. Yani maisha yaniumize kichwa na simba iniumize kichwa siwezi.

Wabakie wanaonufaika na simba ndio waumie sio mimi niliopo nanjilinji ndanindani huku.
🤣🤣🤣Hongera kwa kujitambua
 
Back
Top Bottom