Nyamizi
Platinum Member
- Feb 19, 2009
- 9,186
- 13,757
Hapo pa BlackBerry umenikumbusha mbali sana.Wakati huo zinauzwa aghali na kwa mara ya kwanza napewa ofisini nilikuwa nikipokea simu mbele za watu wananiona wa maana sana maana natumia simu pendwa aliyokuwa akitumia pia Barack Obama kumbe ilikuwa kwa hisani ya Boss Kaburu .Huwa sielewi ilikuwaje soko lake likafa gafla kiasi kile.Facebook imeanzishwa 2OO4 ulaya ila kutufikia sisi huku ilikuwa ni past 2OO7 hivi huyo mtu anaizungumzia kama kitu cha enzi hizo dah [emoji23][emoji23][emoji23]!
Nakumbuka 2004 hadi 2OO6 watu walikuwa wanahangaika na Mig 33 [emoji23][emoji23][emoji23] kwenye nokia zetu pendwa.
Baada ya ios na android kuingia mainstream ndio facebook na whatsapp zikajizolea umaarufu. iOS ilizinduliwa 2007 na android 2008. Blackberry alikuwa moto sana 2010-2012 na BBM yake kabla hajafa kibudu 2022[emoji23]