Wanajamii kama nitakosea mtanikosoa ila kwa kweli kupata idadi kami ni ngumu sana ila nimewahi kufanya utafiti wa hali ya juu saana katika hili la nani ana wapenzi (wanachama)mashabiki wengi kati ya Simba Sport club 'wekundu wa Msimbazi au Dar Young african 'YANGA'Nimebahatika kutembelea na kuishi mikoa na wilaya nyingi za Tanzania bara na visiwani isipokuwa Mkoa wa Katavi tu kwa takwimu yangu isiyo rasmi mikoa yote ya Bara isipokuwa Dodoma,Tanga na Singida ndio Simba inaongoza kwa 60% Lakini iliobaki Yanga wako mbali sana mfano Kagera,Kigoma,Mbeya,Arusha,Mtwara Tabora Mara Hata Pwani wanaweza kufikia hata 70%Mpaka 75% iliyobakia Yanga wanavuna mashabiki wengi tu hata 65% kama Kilimanjaro,Moro,DSM,Shinyanga,Manyara,Iringa,Rukwa,Mwanza,Lindi na Ruvuma upande wa Tanzania visiwani Unguja Yanga wanaongoza kwa wingi ila kwa Pemba wanaweza kulingana au Simba kuzidi kwa thuluthi kadha pia Yanga wana mashabiki lukuki Uganda na maeneo kadha ya pwani ya Kenya. Mombasa,Malindi na lamu. Huenda Yanga wakawa na Mashabiki kwa 40%kwa eneo zima la Afrika mashariki Utafiti huu nimeufanya kati wilaya karibu zote katika mikoa nilio orodhesha hususani katika Viwanja vya Soka. Mara nyingi zinapocheza timu hizo mbili au zikija kupambana na timu za Mikoa hiyo