Simba na Yanga wawaombe radhi Wazanzibari

Simba na Yanga wawaombe radhi Wazanzibari

Mashindano na sherehe za mapinduzi cup yamedoda kutokana na Simba na Yanga kutolewa kwenye hatua za awali za mashindano. Wanasiasa, wanamichezo, wadhamini na wazanzibar wote hawakutendewa haki na Simba na Yanga kupeleka timu dhaifu kwenye mashindano.

Shamrashamra hazitauwepo kamà nusu fainali na fainali hakuna Simba na Yanga, Simba au Yanga.

Viongozi wa hivi vilabu vya Simba na Yanga wahojiwe na wapewe adhabu kwa kuyadharau mashindano.
Ndio mjifunze kupenda na timu zingine pia, sio hizo mbili tuu
 
Shida ni pesa ndio maana Simba na Yanga zimejitoa,gharama wanazotumia ni nyingi kuliko watakachopata.
 
Ni upumbavu mkubwa kupeleka wachezaji muhimu kwenye kombe la milioni 15 halafu wanavunjwa miguu wanakosa michuano muhimu.

Binafsi niliona mwaka jana ujinga huo.
Utopolo kama kawaida yao wakalipa watu wawaumize wachezaji wa Simba kwenye michuano hiyo ili wao wapete kwenye ligi.
Kibaya zaidi walitaka Simba iharibu pia kimataifa.

Nawashukuru viongozi wa Simba kuona hilo.Ni mashindano ya kuoneshana undava undava tu.Waamuzi hawatoi kadi nadhani wana maelekezo.Kwa nini upeleke kikosi muhimu?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
[emoji1787][emoji1787] hii nchi ina mashabiki wajinga sana, yaani yanga ilipe watu kuwavunja wachezaji wa simba![emoji849]
 
Yule Masingisa Mbatta aliondoka Yanga na malalamiko ya timu kuendeshwa kisiasa zaidi kuliko ki professional. Timu inakwendaje kwenye mashindano yanayowatia hasara? Yanayominya muda wa maandalizi ya mashindano mengine? Yanayozalisha majeruhi? Yanayokula muda wa kwenda preseason?

Kosa lao ni kukubali kushiriki halafu hawaendi kushiriki bali kuhudhuria.
Unathibitishaje kama hawashiriki wakati wameingiza timu uwanjani na wachezaji waliocheza niwa timu husika?.Au simba na yanga hazitakiwi kufungwa?
 
Wazanzibar msitulazimishie muungano kupitia mapinduzi cup. Chezeni wenyewe na hako ka nchi kenu kabaguzi. Si mnasemaga ndugu zenu wako Oman na Qatar. Go for them.
Kwanza zawadi yenyewe ni 20+m....ongezeni dau angalau 100+m mpira uchezwe. Sio wachezaji wetu waumie kuwafurahisha wanasiasa.
Kombe lenyewe lina mkosi hilo.
 
Ni siasa tu,lakini ilitakiwa ziende timu ndogo ndogo nao wapate platform ya kuonesha vipaji vya wachezaji..na ingezoeleka hivyo na wala kusingekua na maneno.
Dawa ya muungano ni Tanzania tuwe na ligi moja TU sio hii akadalbla tunayoifanya.
 
Wazanzibar msitulazimishie muungano kupitia mapinduzi cup. Chezeni wenyewe na hako ka nchi kenu kabaguzi. Si mnasemaga ndugu zenu wako Oman na Qatar. Go for them.
Kwanza zawadi yenyewe ni 20+m....ongezeni dau angalau 100+m mpira uchezwe. Sio wachezaji wetu waumie kuwafurahisha wanasiasa.
Kombe lenyewe lina mkosi hilo.
Hawa walijitoa wenyewe kwenye ligi kuu Sasa wanataka ligi kuu kwa njia za ujanja ujanja. Ama kweli watu wa Bara ni mazuzu kwelikweli
 
Yeye kama CEO wa timu jukumu lake lilikua ndo kuibadilisha taasisi kutoka uelekeo wa kisiasa kwenda kiproffesional ndio kazi ambayo aliajiriwa aifanye sasa anamlalamikia nani alitakiwa kuibadilisha iyo hali akiwa ofisini kusema huku nje inakua ndo yale yale ya kinyongo cha mwanamke alieachika ohoo mtu mwenyewe ulikua haunifikishi na blah blah zingine kibao.. hata uko nje uwezi kuona timu inapelekea vikosi vyao vya kwanza kwenye carabao au cop del rey wakijua kuna mashindano ya muhimu mbele yao
Aliondoka baada ya kushindwa kuibadilisha hali, timu imejaa wanasiasa wengi. Ndio maana akabwaga manyanga, na hizo ndizo sifa za kiongozi mahiri.
 
Aliondoka baada ya kushindwa kuibadilisha hali, timu imejaa wanasiasa wengi. Ndio maana akabwaga manyanga, na hizo ndizo sifa za kiongozi mahiri.
Ndo akae kimya sasa, kuweka wazi masuala nyeti ya waajiri wako wa zamani iyo sio proffesionalism
 
Ndo akae kimya sasa, kuweka wazi masuala nyeti ya waajiri wako wa zamani iyo sio proffesionalism
Hii ni tiba ya tatizo. Watu walikuwa wakimlazimisha aseme ni kwanini amebwaga manyanga ghafla. Alificha lakini mwisho alisema kuwa mpira wa Tanzania umechanganyika na saisa sana, mwanzo nilimshangaa lakini baada ya kuona abramovic amenyang,'anywa timu ya Chelsea kwa sababu za kisiasa nikaona kumbe kwenye mpira kuna siasa pia duniani kote.
 
Shida ni pesa ndio maana Simba na Yanga zimejitoa,gharama wanazotumia ni nyingi kuliko watakachopata.
Mpira ni pesa sasa hivi, timu siku hizi zinamiliki vikosi ngali sana kulipa mishahara, signing fee na bonus, kulisha, kusafirisha, kutibu na kuvipatia mahali pa kuishi. Tuondoe siasa siasa na mabonanza kwenye timu zetu hizi. kama mashindano ya mapinduzi ni muhimu lazima mzigo uwekwe pale. Mfano, baadhi ya wadhamini wa mashindano ya mapinduzi walikuwa chuo cha afya kinaitwa City College of Health and Allied Sciences. Chuo kama hiki kutangazwa na kupatiwa milege na timu za Yanga, Simba, Azam na Singida Big Stars kilitakiwa kulipa hela nyingi sana ili kupata nafasi hiyo. Lakini inawezekana imetoa milioni 10 tu kujitangaza kupitia mashindindano yale, NIC na wengine vilevile. Huku ni kuzibaka timu kubwa kama Simba na Yanga. Kama mshindi wa kwanza wa mashindano anapewa 30 m je aliyeshika nafasi ya 6 kalipwa sh ngapi? je, ghrama za timu zimelipwa na nani?
 
Back
Top Bottom