Simba na Yanga zapewa heshima kwa mafanikio na mchango katika kukuza chapa ya Ligi Kuu Bara
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetoa zawadi kwa klabu za Simba na Yanga kama ishara ya kutambua mchango mkubwa katika kutangaza na kukuza chapa ya Ligi Kuu Bara ndani na nje ya bara la Afrika kutokana na mafanikio ya klabu hizo kwenye michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.