Simba na Yanga zimetutia ujinga mwingi

Simba na Yanga zimetutia ujinga mwingi

Kufatilia Simba na Yanga ni moja ya ujinga

Mtu makini anaangilia EPL au LALIGA na sio upuuzi

Nunua Tv yako flat screen nchi 50 nunua DStv yako then watch the game.
Wahaya Mtabadilika lini nyie??? So watugambile stupid mshaija kisa kuangalia ligi ya Tanzania?
 
Kuwa World Cup haimaanishi ina kiwango cha dunia , inategemea ni World Cup ya nini . World Cup zipo nyingi mno na watu hawazijui na si Tanzania tu . Mfano fainali ya UEFA ipo juu mno kuliko World Cup ya basketball. Issue siyo global stage issue ni aina ya mechi .

Jibu langu ni kwamba Simba Vs Yanga bado imeizidi umaarufu hiyo mechi ya mabinti na si huyo mtangazaji pekee bado utaona hata vibanda umiza na pub zitajaa hapo kesho 23 ila Hiyo ya mabinti nani anatizama?
Very Critical.
Timu za Tanzania zinaenda Worl Cup za levels ambazo hazina Mvuto.
Mfano;
World Cup ya Watoto wa Mtaani/Chokoraa.
Word Cup ya Watu wenye Ulemavu.
World Cup ya Viziwi.
World Cup ya Wanawake nk. Sasa mtoa uzi unataka tushabikie vitu ambavyo wenzetu hawspeleki hata timu????
Soooon tutaletewa WORLD CUP YA MAKAHABA NA MASHOGA nauo tutafika Fainali na mtataka tuiongeleee kwenye media.
Kwanini si World Cup ya Timu iliyokamili ya Taifa Stars ndicho Watanzania tunataka! Sio hizo mabonanza hapi juuu.
Anyway Jumapili hakuna MBA MBA MBAAAAAAA
 
Nikisikiliza habari za michezo leo alasiri kupitia chombo kimoja kikubwa cha habari nchini. Mtangazaji wa habari (za michezo) akinadi michezo itakayojiri kuanzia leo hadi wikiendi Jumapili. Ameinadi michezo yote akiutaja mpambano wa Yanga na Simba kuwa ndiyo mchezo mkubwa na unaosubiriwa na wengi.

Kilichonishangaza ni jinsi alivyoshindwa kuelezea uwepo wa mchezo wa timu yetu ya taifa ya wasichana ambayo kesho mchana itatupa karata muhimu ikicheza robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia, ameshindwa hata kuongelea uwepo wa mchezo huo!

Nimejiuliza hivi hizi Simba na Yanga zimetufikisha kutudumaza akili kiasi hiki? Wale mabinti wameweka historia na sasa wao ni gumzo katika tasnia ya michezo duniani, kwa kuwashinda vigogo wakubwa na kutinga robo fainali. Wewe mwandishi huoni kama ni stori badala yake unakazia na kurembesha habari ya Simba na Yanga!

Watanzania tuamke, Watanzania tubadilike, tuangalie mbali, tuangalie Dunia inakwenda vipi, tusidumae akili.
Tuwape hongera na kuwaombea sala na dua vijana wetu wa chini ya miaka 23, wasichana watakaocheza robo fainali na Colombia saa 8 kesho (India) na wale wavulana watakaocheza na Nigeria saa 10 kesho (Dar).


Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Watangazaji wengi hawana taarifa za nje maana hawaijui lugha ya Malkia na si watafiti

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Mtoa mada naomba wewe kama wewe unitajie majina ya wachezaji watano wa hiyo timu ya wanawake na nafasi wanazocheza pamoja na club walizotoka
 
Tatizo ni kwamba wanawake na vilema hawathaminiwi.

Hata soccer yao inaonekana kama si soka kamili.

Na hii si kwenye vyombo vya habari tu, hata kwenye jamii.

Ukisikiliza mazungumzo mengi huwezi kusikua soka la wanawake au walemavu.
 
Back
Top Bottom