Nikisikiliza habari za michezo leo alasiri kupitia chombo kimoja kikubwa cha habari nchini. Mtangazaji wa habari (za michezo) akinadi michezo itakayojiri kuanzia leo hadi wikiendi Jumapili. Ameinadi michezo yote akiutaja mpambano wa Yanga na Simba kuwa ndiyo mchezo mkubwa na unaosubiriwa na wengi.
Kilichonishangaza ni jinsi alivyoshindwa kuelezea uwepo wa mchezo wa timu yetu ya taifa ya wasichana ambayo kesho mchana itatupa karata muhimu ikicheza robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Colombia, ameshindwa hata kuongelea uwepo wa mchezo huo!
Nimejiuliza hivi hizi Simba na Yanga zimetufikisha kutudumaza akili kiasi hiki? Wale mabinti wameweka historia na sasa wao ni gumzo katika tasnia ya michezo duniani, kwa kuwashinda vigogo wakubwa na kutinga robo fainali. Wewe mwandishi huoni kama ni stori badala yake unakazia na kurembesha habari ya Simba na Yanga!
Watanzania tuamke, Watanzania tubadilike, tuangalie mbali, tuangalie Dunia inakwenda vipi, tusidumae akili.
Tuwape hongera na kuwaombea sala na dua vijana wetu wa chini ya miaka 23, wasichana watakaocheza robo fainali na Colombia saa 8 kesho (India) na wale wavulana watakaocheza na Nigeria saa 10 kesho (Dar).
Sent from my SM-A205F using
JamiiForums mobile app