Simba na Yanga zinapaswa kujifunza zaidi fitna za mechi za kimataifa, tulichokiona Sudan ni trailer tu, picha lenyewe linakuja

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Kwanza nikiri mechi ya Jana kati ya Simba na Al hilal sikuangalia Kwa lakini kutokana na mazingira nilikuwa sehemu za kugonga vyombo.

Lakini nimejifunza kitu Watanzania tuna ukarimu wa kiboya sana, tunawakarimu wageni wakija kwetu lakini tukienda kwao ni tofauti.

Kwa mechi kama ya Jana tena friend game sikutarajia kuona tension kama ile kana kwamba kuna kitu mnagombania wakati ni mechi tu za kuangalia vikosi vyenu.

Sasa wahuni kama hawa kama watakuja kukutana na Yanga ni watu wa kumalizana nao Dar, tumechoka ukondoo wa kila siku timu za Tanzania kufanyiwa uhuni ila wao wakija kwetu wana kuwa Salama.

Kama mechi ya Jana ilikuwa si ya kugombea chochote watu wanataka kutoana roho inakuwaje wahuni kama hawa ucheze nao wakiwa wanataka kufuzu?

Tubadilike Sasa tuachane na ukondoo.
 
Ni kweli bhana,, hao wageni wakifika home ni kuwapelekea Moto tu.. Tusikibali kufungwa home kabisa
 
ubora wa uwanjani na nidhamu ndo kitu chamsingi km wachezaji wetu wataleta yale mambo wanayowaletea marefa wetu kutakua na shida, kwanza yanga mi na hofu na beki yetu ya kati tuuu, tumejaza watu mbele but defence yetu huwa inababaika sana tukishambuliwa hasa captain,
 
Hiyo elimu ni ya Yanga Simba anajua kucheza huu mziki unaitwa club bingwa na Shirikisho ndio maana unaona rank yake yumo ndani ya 20,Kwa Al hilal kutolewa na Yanga ni aibu kwao maana Yanga kwenye michuano hii ni underdog kwelikweli ,Al hilal nadhani Kila msimu anacheza makundi ni jambo la kawaida kwao ila kufika Robo kwao imekuwa shida ndio maana wanafukuza kocha kila mwaka Kwa sababu ya kutofika Robo sio kuingia makundi ,kuingia makundi ni lazima sio ombi.Team kama ZAMALEK inaweza isiingie makundi lakini kocha anaangaliwa tu kwao priority ni kuchukua ligi ya Egypt ila sio El mereck na Al hilal hawana mzaa na makundi club bingwa.
 
Naomba
Nipigie kura kwenye chapisho langu la Tanzania yenye sura mbili ndani ya sura moja
 
Baada ya kuona mna mziki huko mbeleni mnajifanya et kuwakazia wageni .
Fans wa yanga wapunguze shobo za kupokea wanaume airport huo ni upimbi na ushamba mkubwa.
Mimi nikifikiria Simba na yanga linapokuja swala la kimataifa wangekua kitu kimoja ,ila ndani ya nchi ndio wafanyiane fitna
 
mashabiki wa utopolo nao waachane na ile tabia yao ya kishamba ya kwenda airport kupokea timu ngeni zinazokuja kucheza na simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…