Simba na Yanga zitaweza ushindani wa Afrika? Al Ahly imemuajiri kocha wa Mamelodi, Mosimane kwa mshahara wa Dola za Kimarekani 120,000 kwa mwezi

Ukiwauliza kuna timu ambayo inakuwa bora misimu yote wanakimbia..

Wao nao wabahatishe sababu timu wanayo.
Tp Mazembe kwanini hawatolewi raundi ya kwanza tu? Au achana na Tp Mazembe ni mbali hao, timu ya hororya kwanini hawajatolewa raundi ya awali tu baada ya kufikia hatua ya robo kama ilivyo kwa Simba?
Hatukatai kuwa timu haiwezi kuwa bora msimu yote lakini ni ajabu Sana kwa timu iliyofika robo fainali msimu uliopita ikaja kutoka hatua ya awali katika msimu unaofuata.
 
Ukiwauliza kuna timu ambayo inakuwa bora misimu yote wanakimbia..

Wao nao wabahatishe sababu timu wanayo.
Timu haiwezi kuwa bora misimu yote lakini pia timu bora haiwezi kuwa bora kwa msimu mmoja tu. Timu ikifanya vizuri kwa msimu mmoja tu basi hakuwa bora bali alifanya vizuri kwa bahati tu. Mfano nakupa

Mwanafunzi anaenda kwenye mtihani na kisha anafanikiwa kuingia katika kumi bora wa wanafunzi wote wa Tanzania na kushika nafasi ya kumi. Huyu mwanafunzi huyo huyo anaamua kujipanga vizuri zaidi ili aje afike tano bora. Lakini ajabu huyu mwanafunzi anakuwa ndio Kati ya wanafunzi wanaoshika nafasi ya mwisho. Hapa unapata picha gani kwa huyu mwanafunzi?

Ndio maana juu kuna mtu juu alitaka umpe takwimu ya Simba kufanya kila msimu unaofuatia baada wa nyuma ulitoka kufanya vizuri ili aone consistency ya Simba kimataifa.

Habari ya wachezaji kuachwa hilo halituhusu kwasababu hakuna kiongozi, shabiki, Wala mpenzi wa Simba aliyetegemea kuona pengo la wachezaji waliyokuwa wameachwa zaidi ya kufarahia usajili na kujisifu kuwa mmeenda next level nakuleta wabrazil. Wewe unazunguzia kikosi hakukuwa bora baada ya kucheza hao wachezaji.

Mimi nazungumzia uboreshaji wa kukosi kimalengo na kimkakati ulifanywa na klabu ya Simba. (Nadhani hata wewe uliamini ni kikosi bora kuliko kikosi cha nyuma yake wakati wa usajili) na ndio maana hakuna aliyepiga kelele juu ya wachezaji waliochwa mpaka mlivyowaona hao wachezaji mapungufu yao.

2) mchezaji aliyefanya vizuri msimu uliopita kuja kufanya tena vizuri msimu unaofuata hiyo ni assumption tu unafanya kwasababu kimpira wanaweza kweli wangefanya vizuri au wasingefanya vizuri pia kwavile ulishasema mpira sio a e i o.
 
Smt016

Elewa kuwa Simba alikuwa bora wakati huo na sio bahati.

Nilikuuliza swali hutaki kujibu unaruka tu na maneno.. (Mechi 10 WIN 6 ni bahati..?

Huo mfano wa mwanafunzi... Wewe hujawahi kusoma na mtu mwenye uwezo halafu kwenye matokeo anashindwa kufaulu?
... Hata kwenye mitihani kuna mambo yanaweza kupita kati ukashindwa kufanya vzr. (najua umesoma unanielewa)
 

Simba vs Mbabane 4:1
Mbabane vs Simba 0:4
Nkana vs Simba 2:1
Simba vs Nkana 3:1
Simba vs Js Soura 3:0
As Vital vs Simba 5:0
Al Ahly vs Simba 5:0
Simba vs Al Ahly 1:0
Soura vs Simba 2:0
Simba vs Tp Mazembe 0:0
Tp Mazembe vs Simba 4:1

1) nakurekehisha Simba kacheza michezo 11, kashinda michezo mitano kafungwa michezo mitano katoa sare moja.
2) bahati ya kwanza inaanzia kwa As Vital kuanza kutoa sare na Soura wakiwa nyumbani kwake. Na hapa ndipo palipo na msingi wa Simba kushika nafasi ya kumfanya avuke hatua ya makundi.

2) timu yenye uwezo haiwezi kufungwa mfululizo magoli 4+ ugenini kila mara, kufungwa magoli mengi ni kuonesha uwezo duni dhidi ya mpinzani wako.

3) kulikuwa na tetesi juu ya Simba kutumia njia zisizo sahihi vyumbani ili kuihujumu timu pinzani. Al Ahly, Nkana, na As Vital waliilalamikia hilo. Ikafikia hadi kuvuma na kupelekea kutokea kwa kauli za ufatiliaji wa hilo tukio kwa mechi iliyofuata ya Simba vs Tp Mazembe, ndipo tunaona kwa Mara ya kwanza Simba anashindwa kupata matokeo ndani ya uwanja wa Mkapa. Vipi Kama hayo matekeo yameshindwa kupatikana kwavile Simba walishindwa kufanya mbinu za nje uwanja kutokana na kutishiwa?

4) nilitoa mfano wa mwanafunzi ukanijibu kuwa sijawahi kuona mwanafunzi mzuri anafeli mtihani.
Mwanafunzi mpaka anaitwa mzuri maanake ameweza kumantain ubora wake kwa kipindi cha muda mrefu. Mfano kwanzia anaanza darasa la kwanza hadi kidato cha nne mtihani wa moko mkoa yeye kwenye tano bora hamkosi, huyu mwanafunzi akitokea kafeli mtihani wa taifa ndio tutasema mwanafunzi mwenye uwezo kafeli.

Sio mwanafunzi anashika nafasi za mwisho weeee kila miaka halafu siku paa inatokea mtihani nae kaonekana kwenye top ten. Mtihani unaofuata tena karudi tena chini kama kawaida yake. Inapita miaka kibao anaubuka tena kwenye top ten. Aisee huyo hana uwezo ni mbahatishaji tu
 
Smt016

Nilisema michezo 10 nikiwa ninamaanisha kabla ya ile 2 ya robo fainali.

Hapo umesahau mchezo wa (Simba 2-1 As Vita) uliompeleka robo fainali.
Ok. amecheza 12 AMESHINDA 6

**KUMBE na wewe uliamini Simba wanapuliza madawa..? (mbona hawakufungiwa)?
 
Mbona Simba wana Viwanja vya mazoezi au ni lazima ukitaka zungumzia moja ya team hizi utaje zote?

Viwanja vya mazoezi hawana watawezaje kumlipa mtu kama huyo?Hivyo vilabu vyote havina watu wa mpira wana watu wa siasa yaani huko wanawaza ccm ndio mpira baada ya miaka miamoja labda wanaweza kupata watu wanaoweza kufikiri namna ya kuendesha mpira
 
Hizi habari za Simba kupuliza Madawa ni sisi yanga tulikubaliana kuzivumisha ili kuwatoa Simba mchezon. Na tulikuwa tunaziambia hata hizi team mapema. Hakukupatikana ushahidi wowote. Kupuliza madawa kwa team hizi kongwe zenye wataalam wa kila nyanja ni kufukia kaburini. Team itafungiwa na kupigwa adhabu kubwa sana. Kuna kipindi.tuweke ushabiki pembeni tukubali uhalisia.
 
Huyu kocha ameshatupiwa virago tayari na Al Ahly!! Walikuwa wanamlipa pesa ndefu huku moyo ukiwauma!! Kwa hiyo walipokosa ubingwa wa Afrika walifurahi kwamba wataitumia hiyo kama fursa ya kuachana na kocha huyo. Mosimane ni bonge la kocha, lakini katupiwa virago!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…